Tukumbushane Kiwanja Ngoma Mbeya!

Tukumbushane Kiwanja Ngoma Mbeya!

sekulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
988
Reaction score
158
Nani ambaye alishawahi kucheza mpira (ligi za watoto) Mbeya, Kwenye kiwanja ngoma.

Mimi nilikuwa nachezea Tim moja ilikuwa inatokea Iyunga, tulikuwa tunajiita Everton. Kiongozi wetu alikuwa anaitwa BENO, mmoja ya Wachezaji tulokuwa nao ni Emannuel Gabriel aliyekuwa anachezea Simba ila Jana nimemuona Arusha.

Tujikumbushe
 
Snow White, Volcano, Forest, Polisi nk umenikumbusha mbali sana.
Kuna timu ilikuwa inatokea Isanga sijui ilikuwa inaitwaje.
Mi nilikuwa shabiki tu.
 
Mimi nilichezea Jogoo Basha na bdae nikacheza Saitama.
 
nilicheza black town na akina mwamba mkumbwa kipindi hicho akina yona mwakalinga ndo walikuwa wametoka kuchujwa,nakumbuka nishawahi kuteguka bega wakati nadaivu kudaka shuti la abdul(said)mtupa dah!!!kitambo sana
 
naskia siku hizi ule uwanja wazee wameweka garden pale wananywea bia!too sad sijui tutawapata wapi akina vicent barnabas wengine tena?
 
Yes nadhani umeisoma, polisi walikua wanajidai sana, eti watoto wa line

Hivi saitama ndo mlikuwa mna mchezaji ambae alikua anashindwa kucheza akiwa amevaa viatu???, unamkumbuka huyu jamaa?? alikua bonge la mshambuliaji

nilicheza black town na akina mwamba mkumbwa kipindi hicho akina yona mwakalinga ndo walikuwa wametoka kuchujwa,nakumbuka nishawahi kuteguka bega wakati nadaivu kudaka shuti la abdul(said)mtupa dah!!!kitambo sana

Yes Black Town naikumbuka, mlikuwa mpo njema!

naskia siku hizi ule uwanja wazee wameweka garden pale wananywea bia!too sad sijui tutawapata wapi akina vicent barnabas wengine tena?

Watoto wenyewe wa miaka hii wanapenda Ngono michezo ipo kwenye Ma play Station

Wazee wetu wenyewe wanapenda Bia!. Kama ni kweli basi manispaa ya Mkoa wa mbeya inatakiwa iwajibishwe kwani pale palikuwa ni sehemu ya watoto kucheza!
 
Yes nadhani umeisoma, polisi walikua wanajidai sana, eti watoto wa line

Hahahaaaa....! Mkuu mie nilikuwa mmoja wa timu ya watoto wa Line, tulikuwa tukienda uwanja ngoma kila mtu alikuwa anatakiwa abebe mkanda wa baba yake wa kazini, timu ilikuwa inatisha wakati huo mimi nilikuwa kipa walikuwa wananiita mtoto wa jini.
 
Timu ya Sheikh Pole, pia ilikuwepo Jah People Barabara ya tano. Ilikuwa kama Yanga.

Jogoo Basha nilikuwa nawekwa benchi, lakini nilifunga goli la kuchukua ubingwa fainali, full maushirikina siku hiyo.
Naklumbuka jaamaa yangu alikuwa kipa na moja ya masharti aliambiwa asishike miamba ya goli, aliposhika tu shuti lililopigwa golini likatinga wavuni
 
Kuna dogo alikuwa anaitwa masoksi, tungekuwa kwenye nchi zinzo thamini michezo yule dogo muda huu angelikuwa Zilionea
 
Dah nakumbuka sana,

Hahahaaaa....! Mkuu mie nilikuwa mmoja wa timu ya watoto wa Line, tulikuwa tukienda uwanja ngoma kila mtu alikuwa anatakiwa abebe mkanda wa baba yake wa kazini, timu ilikuwa inatisha wakati huo mimi nilikuwa kipa walikuwa wananiita mtoto wa jini.

Nyie si mlikuwa mnalinga kwa kuwa watu walikuwa wakisikia mtoto wa line wanajua zikianza fujo, Home Karibu, alafu unajua hofu ya kulala ndani, Duh

Jogoo Basha nilikuwa nawekwa benchi, lakini nilifunga goli la kuchukua ubingwa fainali, full maushirikina siku hiyo.
Naklumbuka jaamaa yangu alikuwa kipa na moja ya masharti aliambiwa asishike miamba ya goli, aliposhika tu shuti lililopigwa golini likatinga wavuni

Mwanangu benchi tena??, Tatizo lilikuwa nini??
Mimi walikuwa wananipanga wakininyima namba nilikuwa nachukia mbaya kabisa, si unajua??, Hiyo ya masharti ni noma

watoto wadogo wachawi, ndo maana soka la bongo halikui

Hiyo ndo hali halisi man uchawi kwenye soka mpaka kwenye mipira ya Makaratasi,

Kuna dogo alikuwa anaitwa masoksi, tungekuwa kwenye nchi zinzo thamini michezo yule dogo muda huu angelikuwa Zilionea

Alafu sijui tatizo nini Tanzania,
 
Mimi nilikuwa timu moja ilikuwa inaitwa Super star winga ya kulia, nilikuwa na jamaa mmoja alikuwa anaitwa Tiba baadaye akaenda ujenzi Rukwa kwa sasa sijui yupo wapi
 
Supa Starrr ahahahahahahahahaaaaaaaaaa, nimekusoma mkuuu!
 
Hiyo ndo hali halisi man uchawi kwenye soka mpaka kwenye mipira ya Makaratasi,

Uchawi kwenye soka yetu ni jadi, wakati huo ilikuwa tunaweka mbufu golini au senti 5 tunaamini ukikaa golini mpira haupiti, namkumbuka Hamad Kapalata alikuwa mfupi lakini machachali.
 
Kuna wadudu flani walikuwa wanajenga kwenye miti ya xmass na walikuwa wanajenga kijumba cha miti unaambiwa kabla ye mechi tulikuwa tunaenda mistuni kutafuta alafu tunaweka kwenye goli. kuna mzee mmoja alituambiaga
 
Kuna dogo alikuwa anaitwa masoksi, tungekuwa kwenye nchi zinzo thamini michezo yule dogo muda huu angelikuwa Zilionea

'masoksi' ndo huyu chalii anyecheza simba hivi sasa mkuku,anaitwa Meshack Abel.alikua na kakae timu moja ya sheik Pole(saitama au santiago ukipenda)aliitwa Reuben.ye alicheza AFC Arusha baadae.kina bantu admin,mbega dafa,boveet al.madogo walinipa raha sana kipindi hicho bana,ila full uchawi!
 
Nilikua natoke sinde ya magereza kipindi hicho pia nilikua shabiki mkubwa wa forest nakumbuka midle alikua akicheza abou kasanga yupo wapi mtu huyu na wote wliomaliza muungano pre school 1993
 
Kuna wadudu flani walikuwa wanajenga kwenye miti ya xmass na walikuwa wanajenga kijumba cha miti unaambiwa kabla ye mechi tulikuwa tunaenda mistuni kutafuta alafu tunaweka kwenye goli. kuna mzee mmoja alituambiaga

Hiyo ndo ilikuwa inaitwa mbufu, tulikuwa tunaiweka golini tukiamini mpira utapita nje tu!! Daa...! Namna gani hapa juju mtindo mmoja.
 
Mgaza, Maya Samson, Meshack Abel, Yona Ndabila, Ebwana vipaji sijui vimeishia wapi. Namsikia Meshack na Ndabila kidogo
 
Back
Top Bottom