Tukumbushane Kiwanja Ngoma Mbeya!

me nlikua nachezea timu ya risons yosso ya magereza pale..............siku tunacheza na SAITAMA wakapaka mafuta ya nguruwe kwenye magoli daaah we acha tu kitambo aaana
 
FOREVER YOUNG.....
Mnanikumbusha mbali sana wana. Nilicheza pale 2001, 2002,2003 ...hamna kama uwanja ngoma
 
Mimi nilikuwa timu moja ilikuwa inaitwa Super star winga ya kulia, nilikuwa na jamaa mmoja alikuwa anaitwa Tiba baadaye akaenda ujenzi Rukwa kwa sasa sijui yupo wapi

Tiba kabla ya Supa staa alivuma sana na volcano. Alikuwa anakaa mitaa ya ghana
 
naskia siku hizi ule uwanja wazee wameweka garden pale wananywea bia!too sad sijui tutawapata wapi akina vicent barnabas wengine tena?

kweli mkuu uwanja wameharibu last month niliuona roho iliniuma sana
 
Mnamkumbuka issah kihange alichezea saitama? Mimi nilikipiga na timu ya MACHINJIONI na refa akionea 2 ilikuwa vurugu mtindo mmoja..
 
Hiyo ndo ilikuwa inaitwa mbufu, tulikuwa tunaiweka golini tukiamini mpira utapita nje tu!! Daa...! Namna gani hapa juju mtindo mmoja.
Hahahahahahaaaaa, kumbe ndo inaitwa mbufu, Duh!
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaaaa..................Sekulu umenikumbusha mbali sana na Kiwanja ngoma.....

Speechless....

Peter Luwungo......Mtoto wa Majengo/Nonde huyu,alikuwa na kipaji huyu dogo,bila kuwasahau Sadik Mwamlima na bwana mdogo Mgaza Mhina.....
 
Binafsi nilicheza pale mwishoni mwa 80s mwanzoni mwa miaka ya 90.......Na nilikuwa nikihudhuria mechi za pale mpaka 1996 bila kukosa,nimesikitika sana kusikia kwamba eti sasa hivi ni garden watu wanakata Kilaji bin Ulabu......Dah
 
Mgaza, Maya Samson, Meshack Abel, Yona Ndabila, Ebwana vipaji sijui vimeishia wapi. Namsikia Meshack na Ndabila kidogo
dogo anakunywa tu mapombe machafu isanga huko,mpira ulishajiishia zamani!yani kama tungekuwa na mfumo wa maana wa kupata wachezaji,sidhani kama East and Central hii kuna vipaji kama vya kwetu!
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaaaa..................Sekulu umenikumbusha mbali sana na Kiwanja ngoma.....

Speechless....

Peter Luwungo......Mtoto wa Majengo/Nonde huyu,alikuwa na kipaji huyu dogo,bila kuwasahau Sadik Mwamlima na bwana mdogo Mgaza Mhina.....
daah mkuu umenikumbusha hawa watu daa! nilikuwa nao secondary mpira wao si mchezo sijui hata wameishia wapikwa sasa!
 
Nimecheza pale, nakumbuka tulikuwa timu moja na Mgaza, jamaa mmoja anaitwa Davi mmasai pamoja na mshikaji mmoja alikuwa nakaa maeneo ya Mbata alishawahi pia kuchezea Tukuyu sars kisha Lipuli ya iringi baadae kidogo alicheza Prison!!

Wapi Shaban Mtupa????
 
Nakumbuka timu ya Nonde ilikuwa na fujo sana, jamaa wakifungwa walikuwa wanarusha ngumi mwamzo mwisho....chini ya timu meneja wao Shuku!!
 
Wakati huo timu ya Forest ndio ilikuwa inasakata kabumbumbu kama Barcelona ya leo!! Chini ya Shaban mtupah na mdogo wake abdul na vijana wengine!!
 
Kulikuwa na mtu anaitwa Denis Joseph, huyu alikuwa hatari tupu japo hakuendelea na soka huyu alikuwa sehemu ya timu ya Meta Sekondari timu iliyokuwa na uwezo wa kucheza ligi kuu, ikiwa na gwala Alan Simumba, baadae ikaundwa timu ya Mzee Mwakasala iliitwa Ngorongoro, ilikuwa na wakali kama Geofrey Mwambona, Keshi, Chiwaya, Daibo, Stan Matola (RIP), hapo Secky(Chambua) alikuwa cha mtoto sana.Hao wote walitimua vumbi pale Uwanja Ngoma.
 
Mimi nilikuwa timu moja ilikuwa inaitwa Super star winga ya kulia, nilikuwa na jamaa mmoja alikuwa anaitwa Tiba baadaye akaenda ujenzi Rukwa kwa sasa sijui yupo wapi
mara ya mwisho nilimsikia akiwa polisi moro,
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaaaa..................Sekulu umenikumbusha mbali sana na Kiwanja ngoma.....

Speechless....

Peter Luwungo......Mtoto wa Majengo/Nonde huyu,alikuwa na kipaji huyu dogo,bila kuwasahau Sadik Mwamlima na bwana mdogo Mgaza Mhina.....

Ndo hivo mkuu tulipofika lazima tukumbuke tuliotoka

Binafsi nilicheza pale mwishoni mwa 80s mwanzoni mwa miaka ya 90.......Na nilikuwa nikihudhuria mechi za pale mpaka 1996 bila kukosa,nimesikitika sana kusikia kwamba eti sasa hivi ni garden watu wanakata Kilaji bin Ulabu......Dah

Ndo utandawazi, Watu wanatamaa mbaya kabisa

dogo anakunywa tu mapombe machafu isanga huko,mpira ulishajiishia zamani!yani kama tungekuwa na mfumo wa maana wa kupata wachezaji,sidhani kama East and Central hii kuna vipaji kama vya kwetu!

Vijana wengi sana tulokuwa nao, kama hawakuendeleaga na shule, basi pombe kwa kwenda mbele!

daah mkuu umenikumbusha hawa watu daa! nilikuwa nao secondary mpira wao si mchezo sijui hata wameishia wapikwa sasa!

Na ndo maana nataka kujua kila mtu atasema lake na utajua nani yupo wapi!

Nakumbuka timu ya Nonde ilikuwa na fujo sana, jamaa wakifungwa walikuwa wanarusha ngumi mwamzo mwisho....chini ya timu meneja wao Shuku!!

Hahahahaha watoto wa nonde walikuwa balaa, mpaka leo nonde ni bad nuz mbaya kabisa man!
 
Kabla ya kuingia uwanjani, wanapiga bulu pale kwa Mwasimba ndipo wanaingia Soko Madwichi.
 
mara ya mwisho nilimsikia akiwa polisi moro,
Duu nimepotezana naye siku nyingi sijui kwasababu niliacha kufuatilia ligi ya nyumbani, kutokana na sababu za ki-psychology. Nani anapenda kuumiza moyo wake mara kwa mara?
 
daah mkuu umenikumbusha hawa watu daa! nilikuwa nao secondary mpira wao si mchezo sijui hata wameishia wapikwa sasa!

Hahaaaaaaaaaaa........
Hope itakuwa ni St. Mary's Queen of the Apostles Seminary Mbalizi(ama Meta?).....Dah.....

Wapi Simwawa,Simelta,Mbwama,Sichundwe,Matema(Nicodemus Mwak
asekele),Castor,Ndesa(Paul),Majembe,Bashosho,Mwanasuwi,Myamba,Robert Mwashemele,Kasomo,Peter Msyani,Seba,Bryson Gama,Gasper(Kahabi) na wengine kibao......Hawa ndio waanzilishi wa SMQASM......

Hapo Rector Fr. Aloyce Mamiro,akisaidiwa na Fr. Andew Lyaunga(Kwikuuuuuuuuuu) na Fr. Adrian Sangu(R.I.P)......

Bila kumsahau mpishi maarufu mzee Gabi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…