Tukumbushane kulipa kodi

Tukumbushane kulipa kodi

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Habari zenu,

Kwanza nianze kwa kusema kuwa sijatumwa wala sina chembe ya uanachama wa itikadi yeyote ya chama cha siasa,mimi ni Mtanzania halali ambaye nimeamua kwa dhati na mahaba kwa nchi yangu kukumbusha wananchi wenzangu.

NCHI HAIJIJENGI
Ipo nadharia moja kwa waliosoma DS vyuoni inasema kuwa maendeleo ni mzunguko(cycle) ikiwa utawekeza kiasi fulani cha mtaji basi tarajia kiasi hicho hicho kama faida yako kwa maana umewekeza milioni 1 basi tarajia faida hiyo hiyo kwenye biashara yako.

Nadharia hiyo siyo kwamba inagusia rasilimali fedha tu,hapana bali hata pia rasilimali watu ikiwa utakuwa na mtaji mdogo au mkubwa wa watu itakupa matokeo ya biashara yako utakayozalisha.

NCHI HAIJIJENGI
Nchi nyingi za ulaya zimepiga hatua kubwa sio kwamba tu,wao ni waanzilishi wa mifumo tunayoishi bali pia ni watekelezaji wakubwa wa mifumo hiyo mfano mwaka 1850's nchi nyingi za ulaya zilifanya Mapinduzi ya viwanda ambavyo imechangiwa na ukuwaji wa soko na kuongezeka kwa wafanyabiashara(wachunguzi) wakienda nchi tofauti kutafuta masoko ya bidhaa lakini awali kulianzishwa sera ya (enclosure system) ambapo tunakadiria kuwa idadi kubwa ya watu walifanyiwa ukatili kwa kuhamisha watu katika mashamba yao ili kuongeza uzalishaji mkubwa wa chakula na malighafi.

Baadae nchi za ulaya zilifanya mabadiliko ya sheria ambayo inayosimamia utozaji wa kodi kwa kila raia ambapo mpaka leo tumerithishwa kutia mifumo yao waliyotupatia baada ya kututawala na baada ya kututawala(SAP).

Msisitizo wangu
Ikiwa nchi ni kama kiwiliwili ambacho kinahitaji huduma ila kuendelea kupata uhai wewe kama mwananchi ambaye inalalamika CCM haijafanya chochote je "wewe umeifanyia nini nchi yako?" Tanzania inayo uwezo wa kuwa miongoni mwa nchi kubwa ambazo zitakazo kuwa na maendeleo ikiwa wananchi watashikamana na serikali zao bila ya hivyo tuendelee kulalamika

#No jobs
#No justice
#No Rights
#No Development
Nchi ipo ndani yako


Wasalamu.
 
Tukumbushane na watumbua kodi pia:

FrPeDpKWIAAlZDe.jpeg
 
Back
Top Bottom