Hii nayo ni kabla ya harusi
1>tatizo ni baba mkwe,mke amenibania.
Sipendwi na wangu wakwe,wote wamenichunia.
Wameamua nifyekwe,mbali kunifutilia.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
2>ndoa yenyewe ni fupi,tena yakimkataba.
Kosa langu lipo wapo wapi,miaka kumi si haba.
Mrefu siyo mfupi,haba na haba kibaba.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
3>ukweli inaniuma,ila siwezi kusema.
Nikisusa ni lawama,ningejitoa mapema.
Nimefeli hii ngoma,kweli sina cha kusema.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
4>mke huyu mke gani,hajafunzwa unyagoni.
Nimwoe nimweke ndani,maji yafike shingoni.
Bora niwache njiani,hata kama nahuzuni.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
5>bora ndoa niizime,harusi nihairishe.
Vyema mimi nikalime,koo nisihatarishe.
Matunda nikayachume,acha wanikaribishe.
Tatizo ni baba mkwe,kupenda posa nyingine.
Shairi=TATIZO NI BABA MKWE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.