Tukumbushane taratibu

Tukumbushane taratibu

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kwa wana JF wenzangu

Najua tuna pata wanachama wapya hapa JF kila siku hivyo nimeona nikumbushe mambo machache hapa

1. Hoja inayolenga kuchafua Biashara/ Brand
Naomba tena niwaombe sana: isiwe kila mtu akiona kasoro flani hata hana hakika kuwa imetoka moja kwa moja kwa mzalishaji anakuja hapa ku attack. Unaweza kusikia Soda flani mbaya au pengine amechanganya chenji kwenye duka anakuja hapa kusema duka flani ni wezi
Naamini kuna Vijana wengi wapambanaji wanajua jinsi ilivyokuwa Ngumu kujenga Brand ya biashara na maanisha kujenga jina na kupata wateja, naomba tusaidiane kusimama ili tuweze kubebana

2. Viongozi wetu wa Kitaifa ni kama kioo cha Nchi hivyo, naomba mtu kabla hajapost chochote cha kuwa beza hata kama kuna kauli hajailewa ataumie busara na sio kushambulia kwa maneno ya kejeli; Kuwa kiongozi wa Nchi haimaanishi kuwa ni Malaika/hawezi kukosea au kuwa na mtazamo tofauti na wakwako

3. Taarifa zinazogusa hisia za watu mf: Kuandika flani anaonewa wakati kesi ipo mahakamani sio sawa hivyo ni vizuri kufikiria vizuri kabla ya kuandika kwa ushabiki labda kama una hoja za msingi za kusimamia unacho kiandika

4. Taarifa nyeti kama mlipuko wa magonjwa, hutolewa na mamlaka maalum hii ni kwa sababu hutakiwa iwe taarifa kamilifu inayo onesha ukubwa wa tatizo kwa Nchi, hatua za kuchukua/zilizochukuliwa nk

5. Taarifa zinazo husu Takwimu; Mtu asiweke takwimu za kughushi kama hana takwimu sahihi’ kwani takwinu feki huweza kuleta taharuki kwa watu
6. Kuposti picha za majeruhi kwenye Ajali, hii ilisha katazwa nimekumbusha tu. Unakuta watu badala wasaidie kuokoa wapo busy kushindana nani atakuwa wa kwanza kupost picha

7. Napendekeze mtu akichangia apendelee kuandika KWA MAWAZO YANGU nikimaanisha kuwa mtu atakiwi atuaminishe kuwa anachofikiria yeye ndio tu sahihi

8. Matusi hayaruhusiwi, hata kama mtu atakuudhi, jitajidi kutumia lugha ya staha kidogo

Mchango wangu kwa leo
 
Hakika... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom