Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Miaka ya nyumba kulikuwa na visa vingi vya watu kuuliwa ama kujeruhiwa na Simba wala watu.
Wengi wa Simba hao walitajwa kuwa si Simba halisi ila walikuwa ni binadamu waliojibadilisha kuwa Simba.
Miaka ya tisini katikati kuna binamu yetu aliliwa na Simba huko Mtwara.
Lilikuwa na story nyingi sana za kustaajabisha za Simba hao.
Miongoni mwa stori hizo ni hii:-
Lilikuwa na jamaa alidhulumiwa shamba lake na tajiri mmoja, Basi akafanya jitihada zote ikiwa ni pamoja na kuushirikisha Uongozi wa juu ya Kijiji, lakini hakupata haki yake kwani bwana tajiri alimwaga fedha huko kwa kila mtu.
Alipo ona hajasikilizwa, akaenda kwa mkuu wa wilaya, na bwana kibopa akaitwa huko, Mambo yakawa yaleyale.
Akaenda mkoani na mahakama zote akazimaliza lakini hakupata haki yake.
Basi akaamua kwenda kuisaka haki zake kwa njia zetu zile ambazo hamna atakayekufinya gerezani.
Akaenda Msumbiji, akapewa dawa na masharti, akaambiwa asile damu ila aparueparue tu.
Basi akaelekezwa namna ya kuitumia dawa hiyo kisha akarudi kijijini kwao.
Basi alipofika kijijini akaenda kumvizoa mbaya wake, akamparuaparia, hakuridhika kwa uchungu na hasira aliyokuwa nayo akamla kabisa akbakiza kichwa tu.
Akarudi kwake akagundua kuwa kavunja sharti la kutokunywa damu.
Akajaribu kujirudisha kuwa binadamu Tena, lakini haikuwezekana.
Akaendelea kuuwa watu Hadi pale naye alipouwa na waganga maana watu wa game reserve walisha mshindwa kwani hakuwa wa kawaida.