Tukutane Chamazi complex, Mtibwa sukari Vs Northern dynamo....mtanange wa kimataifa huu.

kibol

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
4,521
Reaction score
2,747
Mtibwa sukari wana wa madizini kutoka pale turiani morogoro leo watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Northern dynamo kutoka pale Ushelisheli, ikumbukwe kuwa Mtibwa wana zaidi ya miaka 14 hawajashiriki michuano hii ya kimataifa wakati Northern dynamo ndio mara yao ya kwanza kabisa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, tutaendelea kupeana updates mbali mbali za kitakachokuwa kinaendelea pale chamazi complex.

Updates
Dakika 45 za kipindi cha kwanza ndio zimeanza hapa azam complex chamazi.

Updates
13' Mtibwa sukari wanapata goli kupitia kwa Jaffar Kibaya.

Update
15' Mtibwa wanafanya jaribio zuri sana kwenye lango la Northern hapa.

Updates
35' Jaffar Salum Kibaya kwa mara nyingine tena anaiandikia Mtibwa sukari goli la pili hapa.

Updates
44' Northern dynamo wanafanya mabadiliko ya golikipa baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

45' kipindi cha kwanza zinamalizika hapa uwanja wa azam complex chamazi huku Mtibwa ikiwa mbele kwa goli 2-0.

HT Mtibwa 2 Dynamo 0.

Updates
45' za kipindi cha pili ndio zimeanza hapa chamazi complex.

Updates
57' Mtibwa wanapata penati hapa, anayekwenda kupiga penalty ile ni Jaffar Salum Kibaya... Goooooooooo, Mtibwa Sukari wanapata goli la tatu hapa, ni hat-trick kwa kijana wa Mtibwa Sukari Jaffar Salum Kibaya.

Updates
Dakika 90 zimekwisha na dakika +3 zimeongezwa.

Update
Mtibwa anaandika goli la nne kupitia kwa Riphat Msuya, Mtibwa 4.

Updates
FT Mtibwa 4 Northern Dynamo 0.
 
Kwanini mtibwa achezee dar na sio moro?
Nafikiri viwanja vya huko havikidhi vigezo vya kimataifa, lakini pia suala la kibiashara zaidi mkuu, Mtibwa ata game zake za ligi kuu kati yake na Simba pamoja na yanga kazitoa turiani na kuzileta uwanja wa jamhuri morogoro kwasababu ya kibiashara mkuu.
 
Km kibiashara chamazi mbali wangepeleka taifa
 
Km kibiashara chamazi mbali wangepeleka taifa
Pengine ni kwasababu simba inautumia huo uwanja kesho kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya mbabane swallows, mie nime guess tu sina uhakika na hili.
 
Basi msalimie Thobias kifaru lugarambwike kama utafanikiwa kuonana nae
 
Mungu ibariki Mtibwa sukari! Hiki ndio Chuo cha wachezaji Tanzania
 
Mungu ibariki Mtibwa sukari! Hiki ndio Chuo cha wachezaji Tanzania
Upo sahihi kabisa, kama Mtibwa wangekuwa makini, sasa hivi wangekuwa wanaongoza kwa goli 5.
 
Pengine ni kwasababu simba inautumia huo uwanja kesho kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya mbabane swallows, mie nime guess tu sina uhakika na hili.
Hapana, hapo taifa kuna viwanja viwili kama sikosei.
 
Hapana, hapo taifa kuna viwanja viwili kama sikosei.
Upo sahihi mkuu, uwanja wa Uhuru na huu wa kawaida wa taifa, ndio maana nikasema mimi nimeamua ku guess tu sina uhakika.
 
Upo sahihi kabisa, kama Mtibwa wangekuwa makini, sasa hivi wangekuwa wanaongoza kwa goli 5.
Unadhani ni rahisi kiivyo,tusubiri kesho tuone nyie Bi Hindu mtakavyoshinda hizo goal 5.
 
November 27, 2018
Dar es Salaam, Tanzania

Results CAF CONFEDERATION CUP football match :
Mtibwa Sugar 4 - 0 Northern Dynamo

FT 4 - 0

90'
4 - 0
Riphat Khamis


58'
3 - 0
Jaffary Kibaya

HT 2 - 0

35'
2 - 0
Jaffary Kibaya


15'
1 - 0
Jaffary Kibaya
Northern Dynamo FC is a Seychelles based football club, they are in the Seychelles League. The team is based in Glacis, Seychelles in Mahe island.
 
Kesho zamu yenu Mikia,nishaanda jezi ya Mbabane Swaziland
Andaa na ndimu kabisa ili uondoe kichefu chefu hiyo kesho, simba ni mfalme porini na uraiani, simba lunyasi kesho anatafuna mpaka mifupa ya mbabane swallows.
 
Andaa na ndimu kabisa ili uondoe kichefu chefu hiyo kesho, simba ni mfalme porini na uraiani, simba lunyasi kesho anatafuna mpaka mifupa ya mbabane swallows.
Mid sitii neno hapa nasubiri kesho baada ya mchezo tujue mbivu na mbichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…