Tukutane hapa ambao majina yetu ya mwanzo yamekosa umaarufu kabisa, tumebaki kuitwa majina ya ukoo ama ya utani,

Tukutane hapa ambao majina yetu ya mwanzo yamekosa umaarufu kabisa, tumebaki kuitwa majina ya ukoo ama ya utani,

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwangu mimi jina langu la mwanzo limekosa umaarfufu kabisa, ni jina ambalo lipo kwenye vyeti tu na vitambulisho.

Jina langu la ziada ni la kijijini lakini hili halipo kwenye cheti cha kuzaliwa

Shule ya msingi nimeitwa jina la ukoo
Sekondari nimeitwa jina la ukoo
mtaani na nyumani naitwa jina la kilugha
kazini naitwa jina la utani
 
Dah mimi jina langu linapatikana katika wilaya 2 Tanzania nzima au duniani kwa ujumla yani nikilitaja kilamtu anauliza "sasa jina gani hilo" naona jau mpaka natumia jina la utani
 
Binafsi sipend kutumia jina langu harisi napenda kutumia jina la baba yangu.

Na Hili linajulikana kutokana na kazi ninayo ifanya.

Mtu leo akiniuliza unaitwa Nani.? Namtajia jina la mzee
 
Mimi jina langu halisi wanalijua niliosoma nao shule ya msingi tu

Wengine wote wananiita jina la utan mpaka mama angu kila mtu moi
 
Jina langu ninaloitwa silo ambalo niliitwa nikiwa mtoto...hivyo nikawa na majina mawili hili la kikabila likabamba ikabidi niandikishwe hilo...hata cheti cha kuzaliwa nimekipata uzeeni...! Ila nalipenda japo la ajabu
 
Unajikuta unaona so kujitambulisha jina lako mbele ya watu.
 
Ukinitafuta kwa jina langu halisi utanitafuta mpaka ukome, natambulika kwa jina la mzee wangu. Binafsi napenda sana
 
Mimi la Kwangu ni yeboyebo, nadhani katika Kila watanzania 100 lazima apatikane mmoja wa kuitwa hili jina.
 
Mzilankende Mnyago Yeye Alilipenda Jina Lake Hasa Akiwa Karagwe, Kagera
Washobokela !!
 
Peketeje babayake anitwa NJE UKOO wa NAKEMBETWA.

PEKETEJE NJE NAKEMBETWA.
 
Back
Top Bottom