Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Kwahiyo ukilala chini ya uvungu wa gari ndo hawawezi kukushoot?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kabisaaaa na mnajazwa ile mbaya,afu kulikua na utekaji sana pale mto manonga km chache baada ya Isaka, enzi hizo dah

Sent using Jamii Forums mobile app
Chief ilikuwa ni balaa coz lake bus ndio waliokuwa wanatamba njia ile km unakumbuka miaka ya 2000 mwanzoni barabara ya khm, shy ilikuwa haina lami ....mabus mengi walikuwa hawaitaki njia hyo , makonda wa lake bus walinibeba mzobezobe kunitoa kwenye siti wakidai eti siti yangu imeuzwa wakati nimelipa nauli kamili kutokea masumbwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
we jamaa muongo sana
 
Mwaka 2016 saa nane usiku natoka zangu kula bata na wana wa TIA, nina kama mwezi nimenunua mark X.... nafika tazara taa zinawaka red, hamna magari kabisa na malori niya kuhesabu, ile nasubiria zimulike green, akatokea mtu out of nowhere anataka nishushe kioo, ana bonge la panga.. nikajaa wenge, pombe zikaniishia.. jamaa mwingine akatokea upande wa kushoto akaanza kugonga kioo kwa kitako cha bastola... mweeee, nikakanyaga mafuta gari inaondoka kwa speed matata... bahati nzuri nilikua sijaweka P(parking).. kuna semi trailer lilikua linavuka kwenda airport nililikosa kosa kuligonga.. nikanyoosha mijamaa nikaiacha haiamini kama nimeiponyoka... nilipofika buguruni sikujali kama kuna watu na magari wanavuka 24hrs... huyooo mpaka getto Tabata.. !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimechekaaaa mnooooo,,,pole kwakweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Mj1
Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
 
Usikuuu | mchana nahisi hiyo ilikua 'code' ya eneo lenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
10 ndani.
10 nje.

Sent using Jamii Forums mobile app
Eeeeeh bwana hili kundi unalifahamu mkuu??? Liliwahi kuvamia lodge ya home miaka ileeeee naishi home ila cha ajabu yanatembea na mapanga sijui majambia tu hayana bunduki...kumi yanajipanga nje kuangalia usalama na kumi mengine yanazama ndani... Siku hiyo mnyama nimejilaza usiku wa manane kumbe yalishamchorea ramani mshua mmoja alikuja kulala pale lodge na alikua na mpunga wa maana kwenye briefcase yake. Majamaa kuvunja mlango yule manager wa lodge akaanza kupiga kelele za msaada jamaa yakamuwahi alichezea kichapo huku kabanwa mdomo, muda huo nilishafika dirisha kubwa maana dirisha moja la hiyo lodge limeelekea home ila kutokana na kuwepo kwa liukuta lirefu na geti yasingeweza kuingia ndani... Sijui ule ujasiri niliutoa wapi nachokumbuka yaliingia kila chumba na jamaa limoja linaonekana ndio tembo lao lina booooonge la mwili ndio lilikua linajivuta linauvamia mlango unajiachia wenyewe. Wakaingia chumba kimoja wakakuta binti mkali amelala na kichupi tu nikasikia yanasema "Hatujaja kuangalia pichu wala chiu ya mtu hapa tunataka helaaaa tuuuu" basi mnyama si nikaropoka "Wewe hapo nimeona sura yako, na wewe hapo yaani inshort niliwataja kama wanne hivi wakawa wanatafuta sauti inatoka wapi maana mimi nje nawaona ndani maana nje giza ila ndani hawaoni nje sababu ya mwanga ndani. Jamaa kuona vile wakaongea "hoya mfanyieni kazi kuna dogo nje huku ametuchora, weeee kusikia vile acha nipige yowe la hatari nje "Jamani weziiiiiiiiiiiiiii" uzuri jirani yetu ni mwanajeshi mwenye nyota zake tatu akachomoka na bunduki yake usiku ikapigwa hewani "Paaaaaaah" majamaa yakaambiana "Kimenuka wana tusepe" yakakimbia mpaka kesho hata nikikutana nao siwakumbuki maana kwa ule uoga hata sikukariri sura zao kwa umakini ila wamewatesa saaaana wafanyabiashara wa maeneo ya kimara na mbezi miaka ile
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji38][emoji38] 'we tulia tunakuja'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubungo mataa lile gari la crdb, nlikuwa nyuma yake kwenye shuttle tunaelekea mabibo hostel, nlitsman kukimbia ila konda akatuzuia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi mwenyewe lile tukio la ujambazi Ubungo tulikua kwenye basi la nne kutoka kwenye tukio hata wale askari wanapambana tulikua tunashuhudia aiseeee lilikua kama movie aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…