Tukutane hapa wale ambao hatukupenda kuvaa shati lenye nembo (lebo) au tai shuleni.

Bani Israel

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,775
Reaction score
3,593
Habari wana jf kama kichwa cha uzi hapo juu wale ambao tulikuwa na katabia ka kutopenda kuvaa shati lenye nembo ya shule ili tusitambulike kirahisi tunakosoma ama kwa sababu nyingine tofauti.

Binafsi nilikuwa muhanga wa haka katabia wakati naanza O'level form 1 miaka ya nyuma nyuma Nachukia sana kuvaa shati lenye nembo yani nilikuwa sipendi kabisa nilikuwa naenda kibishi bishi sana kimbembe ni baada ya kufika form 3 ambapo mwalimu wa nidhamu alipobadilishwa kutoka yule nilienzoea ambae haakuwa serious sana na ukaguzi wa wanafunzi nje ya makutano ya asubuhi kwani nilikuwa sikai mstarini, sasa huyu ticha mpya alikuwa mnoko alafu ni wa kike tuu tuseme ni mwanamke wa makamo namkumbuka alikuwa akiitwa madam Anna kwanza alikuwa akinilia tyming kila siku akiniona nafanya usafi alafu mstarini hanioni siku moja akaniita akaniuliza "Kwann sionagi sura yako mstarini? Apo mzee nikajichekecha fasta nikamwambia huwa namaliziaga usafi kwani kengele hugonga kazi huwa hazijaisha. ticha akanicheki kisha akaniuliza mbona na shati halina (lebo) akimaanisha nembo nikamwambia sina nilinunua nikapoteza kabla ya kupeleka kwa fundi ndio nilipotaka nyingine nikaambiwa zimeisha ndo mpaka leo nimejisahau akaniambia mbona zipo sasa hivi kanunue nikamwambia madam mm saiv sina hela nikipata ntanunua akasema nakupa wiki 1 jumatano ijayo nikukute mstarini na ukiwa na nembo alafu mbona tai huvai nikamwambia iko kwenye begi sijui kufunga ila nilimdanganya ukweli sikuwa nayo ticha akabaki anacheka akaniambia j5 nikukute ushajua na nembo uwe nayo. sawa!

Basi maisha yakasonga iyo ikafika iyo j5 ilikuwa ndio siku ya ukaguzi na hapo sina nembo wala tai dah sikuwa na jins ikabidi nikae kikauzu mstarini ukafika muda wa ukaguzi sasa hapo ndo kimbebe ilipofika zamu yangu ticha akaniambia tu wewe jeuri eeh tangulia ofisini nikukute nikaenda alipokuja akaniuliza kulikoni au ww ni jauri hutaki kukamilisha sare dah nikajitetea pale sikupata ela ya lebo wakati lebo ni 500 tuu [emoji23][emoji23]
Ticha akatoka akarudi na lebo akaniambia shika hii kesho uje umeishona nikamwambia sawa.. kikasonga kesho akaniita sina lebo akaniambia kama hutakuwa na lebi hufanyi mtihani dah nakumbuka kilikuwa kipindi cha kukaribia mitihani nikamwambia ntashona kesho ila moyoni sikutaka kushona.

Nilichofanya ni kuchukua uzi na sindano nikashona kwa juu ile style ya pazia nikawa nafanya kuitia mfukoni nilipofika shule nikaitoa mzee inapepea kama pazia saa ya ukaguzi walimu walipoona wakabaki tu kucheka kwani nilikuwa najua kujitetea sana kwa uongo sijui nilikuwa napata wapi uongo.. maisha ya skuli noma sana huko mbele mungu alinisaidia nikashona vizuri maisha yakasonga maana jina lilifika mpaka kwa head master sitaki kuvaa lebo nikatishiwa kusimamishwa [emoji23][emoji23]..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…