Joseph Nyoni
Member
- Apr 21, 2024
- 5
- 2
Na Joseph Nyoni
Kama kuna kitu muhimu katika taifa ni idadi ya watu. Ongezeko la idadi ya watu hupelekea taifa kuwa na maendeleo makubwa. Ndiyo maana mataifa mengi ambayo idadi ya watu imeongezeka kwa kasi na maendeleo yamekimbia harakaharaka.
Mfano mzuri ni taifa la China ambalo lilipata uhuru mwaka 1949 limekimbia kiuchumi kutoka kuwa taifa masikini hadi kuwa taifa lenye uchumi mkubwa duniani likiwa nyuma ya taifa la Marekani ambayo ina GDP ya zaidi ya dola trilioni 28 huku China ikiwa inaifuatia ikiwa na zaidi ya dola trilioni 18.
Tanzania ni taifa lenye ukubwa wa square meter 945, 085 na ina idadi ya watu milioni 61, wakati Nigera yenye square meter 923, 770 yaani ndogo kuliko Tanzania ina watu wanaozidi milioni miambili ishirini.
Kama taifa tuweke walau kwa hiki kipindi cha miaka 25 tupate walau idadi ya watu milioni 120. Ili kuweza kupata faida nyingi zinazotikana na ongezeko kubwa la watu duniani.
Tunaweza kujifunza kupitia China ambayo tangu ilipopata uhuru mwaka 1946 ilipromoti sera ya ongezeko la watu na ilipofika mwaka 1979 nchi yao ikawa na watu zaidi ya Bilioni moja kutoka idadi ya watu milioni 540. Japokuwa wamekuwa na sera ya kuzaa mtoto mmoja sasahivi wanataka kuiondoa na hii yote ni tayari wameona hawatakiwi kuwabana watu kuongezeka kwani raia wao siyo lazima tu waishi China. Wanaweza kuongezeka na wakapata fursa ya kutafuta maisha katika mataifa mengine kwani ongezeko lao litawafanya wawe na nguvu zaidi ndani na nje ya nchi yao.
Zifuatazo ni faida ambazo taifa linaweza kuzipata kutoka na na ongezeko kubwa la watu nchini Tanzania:
1. Kuongezeka nguvu kazi
Hakika watu wakiwa wengi kuna idadi kubwa ya wafanyakazi inapatikana kwani hata mataifa yenye teknolojia kubwa yanalia na nguvu kazi ndogo au wingi wa wazee katika mataifa yao. Hivyo nguvu kazi ya kutosha ni faida kubwa kwa taifa.
2. Kuongeza masoko
Hakika moja ya vitu ambavyo huweza kuisaidia nchi kukua ni masoko. Tunaweza kujifunza hili kupitia mataifa yenye idadi kubwa ya watu. Wateja wakubwa wa bidhaa huwa ni watu wa ndani ya nchi na tunaweza kuona hili hapa kwetu mikoa yenye watu wengi kama Dar es salaam kuwa mzunguko wa pesa ni mkubwa na chakula hununuliwa kwa wingi mikoani na kuletwa Dar es salaam. Kama haitoshi viwanda vya nyumbani huweza vikapata soko kubwa ndani kabla hata ya kuuzwa nje ya nchi hivyo kuongeza pato kwa makampuni madogo na makubwa na mwishowe kupelekea kukua kwa mitaji.
3. Vipaji huwa vingi.
Watu wanapokuwa wengi, vipaji huwa vingi. Hivyo tunaweza kupata wagunduzi na vipaji vingine, mfano mzuri ni taifa la Nigeria ambalo tunawaona wengi kila sekta. Ukiwnzia kwenye uchumi utakuta matajiri wengi Afrika hutokea Nigeria, kwenye maswala ya taaluma mbalimbali kama afya na fani nyingine utawakuta maprofesa na madaktari kibao, achilia mbali fani ya uigizaji na muziki ndiyo usiseme.
4. Kuongeza wajasiramali na wafanyabiashara.
Wingi wa watu hufanya watu kuwa na mahitaji makubwa kama chakula, mavazi, nakadhalika hivyo watu wengi wataingia kwenye shughuli za ujasiriamali na biashara ili kuweza kuwafanya watu wakidhi mahitaji.
5. Kutangaza nchi kwa nguvu.
Taifa linapokuwa na watu wengi hushuhudia mamilioni ta watu yakishiriki kwenye shughuli nyingi hivyo wingi wao huweza kuwafanya waweze kufika kwa wingi hata mataifa mengine na kujikuta wakilitangaza taifa vema. Leo hii tunawaona wachina, wanaijeria, wahindi mataifa mengi ulimwenguni wakijishughulisha na shughuli nyingi hivyo wingi wao huwafanya wasambae maeneo mengi duniani kutafuta maisha. Kwasababu ni wengi basi Ni rahisi hata Kuonekana wengi kimataifa.
6. Kukua kwa uzalishaji
Mataifa yenye idadi kubwa ya watu hupelekea kukua kwa uzalishaji. Litazame taifa la Nigera ambalo linaonekana kuyaacha mataifa mengine ya Afrika au tunaweza kulitazama taifa la Ethiopia ambalo leo hii pato lake la taifa limekwishafikia zaidi ya $ 120 Bilion na kuiacha Kenya nyuma ambayo ina pato la $113 Bilion ambayo ilikuwa juu ya Kenya zamani. Kwani Ethiopia ina zaidi ya watu milioni 120 wakati sisi Tanzania tuko milioni 61. Tunasababu ya kuongezeka.
Wakati tunafanya ongezeko tunatakiwa kupima ardhi na kuipanga ili isije ikatupa shida baadaye.
7. Kuongeza nguvu ya nguvu ya ushawishi. Kama taifa litakuwa na idadi kubwa ya watu basi taifa litakuwa na ushawishi mkubwa kwani watu wengine watategemea taifa hilo kwa masoko hivyo wataliona fursa na kufanya lisikilizwe na mataifa jirani na hata yale mataifa makubwa. Pia uwepo wa raia wake nje kutaongeza fursa kwani mataifa mengine wataliona taifa hilo ni miongoni mwa taifa lenye watu wanaochochea maendeleo katika taifa hilo.
8. Kukua uchumi kwa kasi.
Mataifa mengi yenye idadi kubwa ya watu yamekua sana kiuchumi. Hivyo Tanzania ikiwa na watu wengi zaidi itegemee kukua zaidi kiuchumi kwani biashara nyingi zinachangamka nchini. Mataifa kama Nigeria, India, Indonesia, pamoja na China yamesaidiwa sana kukua.
Hivyo basi miongoni mwa vitu vya msingi ambavyo taifa hili kuelekea miaka 24 ijue inatakiwa kuvipa nguvu ni ongezeko la watu. Kwani itasaidia kulifanya taifa la Tanzania kuwa kubwa zaidi kiuchumi Afrika na hata nje ya Afrika. Lakini ongezeko hilo lifanyike kitaalamu kwa kuangalia mahitaji ya idadi hiyo kubwa ya watu.
Na Joseph Nyoni.

Upvote
2