SoC02 Tukuze Uchumi wa kila Mtanzania kwa kuboresha Huduma za Afya

Stories of Change - 2022 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Kama ningepata nafasi ya kuboresha kitu kimoja hapa Tanzania, ingekuwa fursa kwa watu wengi kuinua kiwango cha maisha. Kitu ambacho ningeboresha ni mfumo wa huduma za afya, ambapo ningezipeleka mashinani (ngazi ya kijiji/mtaa), ili watu wengi wafikiwe.

Pamoja na jitihada za serikali kutoa huduma za afya kwa kila mtu Tanzania, kuna changamoto mbalimbali, kama zilivyotajwa kwenye makala ya mkakati wa taifa wa afya (kidigitali), 2012 – 2018 (“Tanzania National ehealth Strategy 2012 – 2018 paper”), ambazo ni pamoja na upungufu wa wataalamu wa afya katika ngazi zote kwenye mfumo wa afya; uhaba wa madawa, vifaa tiba, na miundombinu katika vituo vya afya na hospitali. Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika “Wiley Online Library” Tarimo na wenzake, (2018), anasema, takwimu za mwaka 2018, zimebaini kwamba nchini Tanzania, daktari 1 anahudumia watu 20,000, tofauti na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (“WHO”), ambapo daktari 1 anapaswa kuhudumia watu 4000.

Inawezekana Watu wa Kawaida kutoa Huduma za Afya kule walipo?
Mfumo ninaoupendekeza umefanikiwa sehemu mbalimbali, kwa kuwezeshwa na Asasi za Kiraia, zikishirikiana na wataalamu wa afya wa serikali.

Nitatoa mifano miwili. Katika wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, shirika la “World Vision” likifadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Canada lilianzisha mradi uliojikita katika maeneo yafuatayo: Kilimo Endelevu, Mazingira, Elimu, Maji Safi na Salama, na Afya ya Msingi. Mradi ulianza mwaka 1996 na kuhitimishwa mwaka 2004, ambapo ulitekelezwa kwa awamu tatu, (kila awamu ikiwa ni miaka mitatu).
Shirika la “World Vision” lilishirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Nzega, kutathmini tarafa zote za wilaya, na hatimaye Mwakalundi ikachaguliwa, baada ya kukidhi vigezo.

Mradi ulishirikiana na wataalamu wachache wa afya kuanzia ngazi ya wilaya hadi vijijini katika utekelezaji wa kazi zote za mradi. Wakunga wa Jadi walifundishwa namna ya kutoa huduma za uzazi salama. Kwa kutambua kwamba wakunga wa jadi wana ujuzi wa asili wa kuzalisha, mradi uliwaongezea ujuzi wa kisasa, kuwawezesha kupata vifaa muhimu vya kuzalishia; na kuwahimiza kuwapeleka wateja wao (wajawazito) katika vituo vya afya, hasa wale wenye matatizo ya kujifungua.

Wahudumu wa Afya walifundishwa kutoa huduma za msingi za afya, ikiwa ni pamoja na kuzuia na kutibu malaria, homa ya matumbo, kuhara, na mengine. Vile vile, wahudumu wa afya, waliwezeshwa kutoa huduma za afya kwa mama na mtoto, ikiwa ni pamoja na huduma ya chanjo kwa watoto chini ya miaka 5, na akina mama.
Kumbuka, watoa huduma hawa ni wa kujitolea (hawalipwi mishahara), walipewa posho ndogo na mradi kila mwezi, na jamii ilihamasishwa kutoa motisha mbalimbali.

Picha 1: Mhudumu wa Afya akitoa elimu ya afya ya msingi kwa jamii katika moja ya vijiji nchini Tanzania.

Wahudumu wa Afya I Aug 2022.jpg

Picha kwa hisani ya “CHW Central – A global resource for and about Community Health Workers” (Disemba, 2020).

Ili kupanua wigo wa kutoa huduma za afya, mradi kwa kushirikiana na wataalamu wa afya, uliwezesha kuundwa kwa vikundi vya wanawake vya afya, walau viwili kila kijiji. Vikundi hivi, kwa kiasi kikubwa vilifundishwa na Wahudumu wa Afya, chini ya usimamazi wa Wataalamu wa Afya.

Picha 2: Mhudumu wa Afya akimpima malaria mtoto katika moja ya vijiji nchini Zambia.
View attachment 2330401
Picha kwa hisani ya “World Vision – Zambia (Aprili, 2022)

Kwa kipindi kifupi (chini ya miaka mitano) cha mradi, juhudi hizi zilileta matokeo makubwa sana, magonjwa mengi yalipungua (yakiwemo yale ya kuharisha na malaria), vifo vya watoto wachanga na kina mama vilipungua sana. Na hivyo tarafa ya Mwakalundi, ikawa juu ya tarafa zote nne za wilaya ya Nzega (ilhali ilikuwa ya mwisho kabla ya mradi) kwa mujibu wa vigezo vya maendeleo vya “World Vision”, hasa katika eneo la afya.

Picha 3: Wakunga wa Jadi wakishiriki katika mkutano uliojumuisha wataalam wa afya na baadhi ya viongozi wa serikali huko Kivunge, mkoa wa Kaskazini “A” Unguja, kisiwani Zanziba.
View attachment 2330402
Picha kwa hisani ya Maelezo Zanziba, (2014).

Mradi mwingine, ambao nilibahatika kuutembelea upo nchini India, katika mji wa Jamkhed, wilaya ya Ahmednagar katika jimbo la Maharashtra. Ni mradi unatekelezwa na Asasi ya Kiraia inayojulikana kama “Comprehensive Rural Health Project (CRHP)” ambao una wafadhili mbalimbali. Mradi unatekelezwa katika maeneo yanayoshabihiana na mradi wa Nzega kama nilivyoulezea hapo juu.

Ni mradi uliofanikiwa sana kuwezesha jamii katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ahmednagar kupiga hatua kubwa ya maendeleo, hasa katika eneo la afya. Ni mradi uliowezesha watu wa kawaida vijijini kutoa huduma muhimu za afya kwa jamii, ambazo kwa kawaida hutolewa katika vituo vya afya na hospitalini.

Serikali inatambua wasaidizi hawa wa (Wahudumu wa Afya na Wakunga wa Jadi), na ina miongozo mizuri ya kuwajengea uwezo. Changamoto ni kufikisha huduma hii katika maeneo mengi, hasa vijijini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), 2002, zifuatazo ni baadhi ya tabia za jamii yenye afya: mazigira ni safi na salama; mazingira yanakidhi mahitaji ya msingi ya kila mtu; mazingira yanayoshajihisha amani na mshikamano na kila mtu anashirikishwa; kuna uelewa wa maswala ya afya na mazingira; jamii inashiriki kutambua suluhu ya changamoto zao; jamii ina uzoefu mbalimbali na kuna mawasiliano miongoni mwao; huduma za afya ni sahihi na zinapatikana; na kuna matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo kwa wote.

Jamii yenye tabia zilizotajwa hapo juu, inaweza kupatikana, endapo huduma muhimu (hasa za afya) zinapatikana kupitia wawezeshaji wa jamii hasa katika maeneo ya mashambani.

Eneo lingine ambalo wawezeshaji wa jamii wanafanya vizuri, ni elimu ya Afya ya Uzazi na lishe bora.

Mapendekezo
Serikali iimarishe mfumo wa afya vijijini, kwa kuwawezesha wawezeshaji wa jamii.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itathmini miradi iliyotekelezwa na asasi za kiraia ikafanikiwa, na kuona namna ya kushirikiana nazo kupanua huduma katika maeneo mengi.

Serikali itoe kandarasi kwa asasi za kiraia, ili ziwezeshe utoaji wa huduma za afya hasa katika maeneo ya vijiijini. Hii itapunguza utegemezi wa wafadhili wa nje ya nchi ambao ni wachache na hutoa fedha kidogo.

Hitimisho
Kuna haja ya serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuwekeza kwa rasilimaliwatu iliyopo vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za afya.

Rejea
[/URL]

Shirika la Afya Duniani - WHO (2002), “A guide for communities and Community health workers”

Tanzania Ministry of Health and Social Welfare (2013), “Tanzania National eHealth Strategy 2012 – 2018”

www.jamkhed.org
 
Attachments

  • Wahudumu wa Afya I Aug 2022 II.jpg
    Wahudumu wa Afya I Aug 2022 II.jpg
    42.1 KB · Views: 6
Upvote 12
Ili kuweza kupungukiwa na tatizo la kukosa huduma za afya katika jamii, serikali kupitia wahudumu wa afya washirikiane na raia wa kawaida wanaoweza kutoa huduma, kwa kufanya hivyo tutaweza kukuza uchumi wa mtanzania, pia itasaidia kuweza kuwafariji wale ambao walikua na ndoto za kuwa madaktari ila hawakuwa kwasabu ya kipato kidogo, kwani watakuwa wanahudumia wateja wao kupitia elimu ndogo waliyopewana wahudumu wa afya.
 
Ni kweli kuna watu ambao wanaweza kutoa huduma ya afya vizuri tu kama wakipewa darasa kidogo kuhusiana na magonjwa kadhaa.
Hakika, wahudumu hawa (ambao ni wa kujitolea) hufanya makubwa sana katika sekta ya afya, kwani hutoa chanjo kwa akina mama na watoto (hasa wale wa chini ya miaka 5); pamoja na kuzuia na kudhibiti maradhi mengi ambayo husababisha hospitali na vituo vya afya kufurika wagonjwa. Wahudumu hawa wakitumiwa vyema, serikali itaokoa fedha nyingi sana, ambazo zinaweza kupelekwa katika sekta nyingine kusisimua uchumi wa nchi.
 
Ili kuweza kupungukiwa na tatizo la kukosa huduma za afya katika jamii, serikali kupitia wahudumu wa afya washirikiane na raia wa kawaida wanaoweza kutoa huduma, kwa kufanya hivyo tutaweza kukuza uchumi wa mtanzania, pia itasaidia kuweza kuwafariji wale ambao walikua na ndoto za kuwa madaktari ila hawakuwa kwasabu ya kipato kidogo, kwani watakuwa wanahudumia wateja wao kupitia elimu ndogo waliyopewana wahudumu wa afya.
Kweli kabisa, Wawezeshaji wa jamii (hasa wa afya), huona fahari kutoa huduma hizi kwa wananchi, kwani hupewa heshima ya kipekee na jamii husika. Ndio maana huridhia kufanya kazi hizi kwa kujitolea (bila mshahara), bila manunguniko yoyote.
 
Huduma za afya ni za shida sanaa kwenye nchi yetu hasa kwa wakina mama wajawazito.
Ni kweli, hata tafiti mbalimbali za afya zinadhihirisha ukweli huu. Ndio maana nimependekeza serikali ishirikiane kwa karibu zaidi na asasi za kiraia, na ikiwezekana izipe kandarasi za kutoa huduma za afya (hasa maeneo ya vijijini), kupitia wawezeshaji hawa afya.
 
Ni kweli kuna watu ambao wanaweza kutoa huduma ya afya vizuri tu kama wakipewa darasa kidogo kuhusiana na magonjwa kadhaa.
Wapo wengi sana wanasubiri fursa kama hizi. Nimefanya kazi katika miradi ya jamii, watu wengi (wanawake kwa wanaume) wenye viwango mbalimbali vya elimu hukubali kwa shauku kuchaguliwa/kuteuliwa na jamii kushika nafasi mbalimbali za kutoa huduma.
 
Kweli kabisa, Wawezeshaji wa jamii (hasa wa afya), huona fahari kutoa huduma hizi kwa wananchi, kwani hupewa heshima ya kipekee na jamii husika. Ndio maana huridhia kufanya kazi hizi kwa kujitolea (bila mshahara), bila manunguniko yoyote.
Hilo ni la kweli, sasa ni wakati wa serikali kuweza kuwawezesha hawa watu wa kujitolea ili kuweza kunufaisha pande zote mbili (serikali na wahudumu wa kujitolea) na hivyo kusisimua uchumi wa nchi.
 
Sawa! Uzuri ni kwamba mfumo huu wa kuwa na wawezeshaji ngazi ya kijiji ni wa serikali, hivyo ni jukumu lake kuhakikisha unafanya kazi na kuleta tija.
 
Kama ningepata nafasi ya kuboresha kitu kimoja hapa Tanzania, ingekuwa fursa kwa watu wengi kuinua kiwango cha maisha. Kitu ambacho ningeboresha ni mfumo wa huduma za afya, ambapo ningezipeleka mashinani (ngazi ya kijiji/mtaa), ili watu wengi wafikiwe.

Pamoja na jitihada za serikali kutoa huduma za afya kwa kila mtu Tanzania, kuna changamoto mbalimbali, kama zilivyotajwa kwenye makala ya mkakati wa taifa wa afya (kidigitali), 2012 – 2018 (“Tanzania National ehealth Strategy 2012 – 2018 paper”), ambazo ni pamoja na upungufu wa wataalamu wa afya katika ngazi zote kwenye mfumo wa afya; uhaba wa madawa, vifaa tiba, na miundombinu katika vituo vya afya na hospitali. Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika “Wiley Online Library” Tarimo na wenzake, (2018), anasema, takwimu za mwaka 2018, zimebaini kwamba nchini Tanzania, daktari 1 anahudumia watu 20,000, tofauti na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (“WHO”), ambapo daktari 1 anapaswa kuhudumia watu 4000.

Inawezekana Watu wa Kawaida kutoa Huduma za Afya kule walipo?
Mfumo ninaoupendekeza umefanikiwa sehemu mbalimbali, kwa kuwezeshwa na Asasi za Kiraia, zikishirikiana na wataalamu wa afya wa serikali.

Nitatoa mifano miwili. Katika wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, shirika la “World Vision” likifadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Canada lilianzisha mradi uliojikita katika maeneo yafuatayo: Kilimo Endelevu, Mazingira, Elimu, Maji Safi na Salama, na Afya ya Msingi. Mradi ulianza mwaka 1996 na kuhitimishwa mwaka 2004, ambapo ulitekelezwa kwa awamu tatu, (kila awamu ikiwa ni miaka mitatu).
Shirika la “World Vision” lilishirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Nzega, kutathmini tarafa zote za wilaya, na hatimaye Mwakalundi ikachaguliwa, baada ya kukidhi vigezo.

Mradi ulishirikiana na wataalamu wachache wa afya kuanzia ngazi ya wilaya hadi vijijini katika utekelezaji wa kazi zote za mradi. Wakunga wa Jadi walifundishwa namna ya kutoa huduma za uzazi salama. Kwa kutambua kwamba wakunga wa jadi wana ujuzi wa asili wa kuzalisha, mradi uliwaongezea ujuzi wa kisasa, kuwawezesha kupata vifaa muhimu vya kuzalishia; na kuwahimiza kuwapeleka wateja wao (wajawazito) katika vituo vya afya, hasa wale wenye matatizo ya kujifungua.

Wahudumu wa Afya walifundishwa kutoa huduma za msingi za afya, ikiwa ni pamoja na kuzuia na kutibu malaria, homa ya matumbo, kuhara, na mengine. Vile vile, wahudumu wa afya, waliwezeshwa kutoa huduma za afya kwa mama na mtoto, ikiwa ni pamoja na huduma ya chanjo kwa watoto chini ya miaka 5, na akina mama.
Kumbuka, watoa huduma hawa ni wa kujitolea (hawalipwi mishahara), walipewa posho ndogo na mradi kila mwezi, na jamii ilihamasishwa kutoa motisha mbalimbali.

Picha 1: Mhudumu wa Afya akitoa elimu ya afya ya msingi kwa jamii katika moja ya vijiji nchini Tanzania.

View attachment 2330399
Picha kwa hisani ya “CHW Central – A global resource for and about Community Health Workers” (Disemba, 2020).

Ili kupanua wigo wa kutoa huduma za afya, mradi kwa kushirikiana na wataalamu wa afya, uliwezesha kuundwa kwa vikundi vya wanawake vya afya, walau viwili kila kijiji. Vikundi hivi, kwa kiasi kikubwa vilifundishwa na Wahudumu wa Afya, chini ya usimamazi wa Wataalamu wa Afya.

Picha 2: Mhudumu wa Afya akimpima malaria mtoto katika moja ya vijiji nchini Zambia.
View attachment 2330401
Picha kwa hisani ya “World Vision – Zambia (Aprili, 2022)

Kwa kipindi kifupi (chini ya miaka mitano) cha mradi, juhudi hizi zilileta matokeo makubwa sana, magonjwa mengi yalipungua (yakiwemo yale ya kuharisha na malaria), vifo vya watoto wachanga na kina mama vilipungua sana. Na hivyo tarafa ya Mwakalundi, ikawa juu ya tarafa zote nne za wilaya ya Nzega (ilhali ilikuwa ya mwisho kabla ya mradi) kwa mujibu wa vigezo vya maendeleo vya “World Vision”, hasa katika eneo la afya.

Picha 3: Wakunga wa Jadi wakishiriki katika mkutano uliojumuisha wataalam wa afya na baadhi ya viongozi wa serikali huko Kivunge, mkoa wa Kaskazini “A” Unguja, kisiwani Zanziba.
View attachment 2330402
Picha kwa hisani ya Maelezo Zanziba, (2014).

Mradi mwingine, ambao nilibahatika kuutembelea upo nchini India, katika mji wa Jamkhed, wilaya ya Ahmednagar katika jimbo la Maharashtra. Ni mradi unatekelezwa na Asasi ya Kiraia inayojulikana kama “Comprehensive Rural Health Project (CRHP)” ambao una wafadhili mbalimbali. Mradi unatekelezwa katika maeneo yanayoshabihiana na mradi wa Nzega kama nilivyoulezea hapo juu.

Ni mradi uliofanikiwa sana kuwezesha jamii katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ahmednagar kupiga hatua kubwa ya maendeleo, hasa katika eneo la afya. Ni mradi uliowezesha watu wa kawaida vijijini kutoa huduma muhimu za afya kwa jamii, ambazo kwa kawaida hutolewa katika vituo vya afya na hospitalini.

Serikali inatambua wasaidizi hawa wa (Wahudumu wa Afya na Wakunga wa Jadi), na ina miongozo mizuri ya kuwajengea uwezo. Changamoto ni kufikisha huduma hii katika maeneo mengi, hasa vijijini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), 2002, zifuatazo ni baadhi ya tabia za jamii yenye afya: mazigira ni safi na salama; mazingira yanakidhi mahitaji ya msingi ya kila mtu; mazingira yanayoshajihisha amani na mshikamano na kila mtu anashirikishwa; kuna uelewa wa maswala ya afya na mazingira; jamii inashiriki kutambua suluhu ya changamoto zao; jamii ina uzoefu mbalimbali na kuna mawasiliano miongoni mwao; huduma za afya ni sahihi na zinapatikana; na kuna matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo kwa wote.

Jamii yenye tabia zilizotajwa hapo juu, inaweza kupatikana, endapo huduma muhimu (hasa za afya) zinapatikana kupitia wawezeshaji wa jamii hasa katika maeneo ya mashambani.

Eneo lingine ambalo wawezeshaji wa jamii wanafanya vizuri, ni elimu ya Afya ya Uzazi na lishe bora.

Mapendekezo
Serikali iimarishe mfumo wa afya vijijini, kwa kuwawezesha wawezeshaji wa jamii.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itathmini miradi iliyotekelezwa na asasi za kiraia ikafanikiwa, na kuona namna ya kushirikiana nazo kupanua huduma katika maeneo mengi.

Serikali itoe kandarasi kwa asasi za kiraia, ili ziwezeshe utoaji wa huduma za afya hasa katika maeneo ya vijiijini. Hii itapunguza utegemezi wa wafadhili wa nje ya nchi ambao ni wachache na hutoa fedha kidogo.

Hitimisho
Kuna haja ya serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuwekeza kwa rasilimaliwatu iliyopo vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za afya.

Rejea
[/URL]

Shirika la Afya Duniani - WHO (2002), “A guide for communities and Community health workers”

Tanzania Ministry of Health and Social Welfare (2013), “Tanzania National eHealth Strategy 2012 – 2018”

www.jamkhed.org
Afya ni nguzo kuu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi. Huduma za afya zikiwa shirikishi zitapatikana kwa gharama nafuu na hivyo kuleta tija, kwa mwananchi na kwa nchi.
 
Kati ya mambo yanayowekewa bajeti kubwa kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa, ni yale ya afya! Sekta hii ikiangaliwa upya na ikawa shirikishi, jamii na serikali zitaokoa kiasi kikubwa .cha fedha!
 
Swala la afya ni nyeti kwa kila familia. Watoa huduma wakiwa karibu, ni faraja kwa kila kaya!
 
Back
Top Bottom