A
Anonymous
Guest
Naomba niwasilishe changamoto zetu kwa mamlaka husika kupitia nyie ili tupate ufafanuzi wa kulipwa gharama tunazowadai chuo.
Wanafunzi wa Chuo cha Udaktari St. Francis (Morogoro, Ifakara) tulipokea taarifa ya kuitwa chuoni siku ya jumatatu bila kukosa wakati tupo likizo bila kuambiwa sababu ya msingi (nimeambatisha barua ya wito hapo chini). Ila tuliambiwa ni mambo ya kitaalumu tuu yakukijenga chuo chetu na pia gharama zetu watazirudisha ikiwemo nauli na malazi tutakapofika chuoni muhimu tuje na ticketi ya basi na kufika siku husika.
Tulipofika chuoni tuliambiwa ni kwasababu mitihani ya somo la psychology imepotea na hivyo tunatakiwa kurudia hilo somo na pia hakuna refund yoyote chuo itafanya juu ya gharama zetu tulizotumia maana tatizo hilo limetokea sio kwa mapenzi ya chuo.
Tulipouliza mamlaka husika tatizo ambalo sio la kwetu linatuingizaje gharama kubwa hivi na wakati uongozi wa chuo walituahidi nauli zetu watarudisha gharama tulizotumia huku wazazi wetu walikopa wakijua tutarudishiwa nauli, hatujapewa majibu ya kuridhisha.
Na pia tulipouliza kwa wanafunzi ambao hawajafika kwasababu ya changamoto ya nauli kwao itakuaje, tumeishia kuwambia kuambiwa watafanya mtihani huo mwezi wa tisa kama special exam, na hili siyo sawa pia sababu kosa halikuwa za kwao na huwezi kuwaadhibu sababu ya wao kukosa nauli.
Najikuta nabaki na maswali mengi bila majibu;

- Chuo hakina utaratibu maalumu ya kukagua mitihani hiyo wakati inakusanywa kama imetimia?
- Je, chuo hakina chumba maalumu wa kutunza mitihani baada ya kukusanywa?
- Je, wanafunzi huwa tunatoa kila mwaka hela ya tahadhari ambayo ni 50,000/= matumizi yake ni nini kama chuo hakiwezi kutupa fidia angalau hata nusu ya gharama tulizotumia katika usumbufu huu?