Tulianza na Freemason sasa tunaendelea na upinde wa mvua

Tulianza na Freemason sasa tunaendelea na upinde wa mvua

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Kama Matahira ... Huwa hatuna tunalojua. Tunapewa na kupokea na kushika kidedea. Upinde wa Mvua upo miaka mingi kabla hata Ushoga hauja wa maarufu.

Leo ukiona mchoro au picha ya upinde wa mvua mtu anakwambia ni ushoga. Mimi nimekulia Tanga kuna mashoga toka miaka ya 80 huko hata hawakuwa wanaujua upinde wa Mvua.

Nikawaza hivi hao Maharamu wangeamua alama yao iwe ni jua au mwezi ingekuaje? Ingekuwa jua likichomoza tu tunakimbilia ndani au mwezi ukichomoza tunawakimbiza watoto ndani?

Sasa ikitokea movie, cartoons za rangi za watoto kuna upinde wa mvua watu wanakimbilia kuzungumzia ushoga n.k yaani watu kadhaa maharamu wamekaa wameamua kuweka tafsiri waliyotaka wao ya kishetani kwenye jambo la asili nasi hatutumii akili tunabebana nalo kila wakati.

Kama ilivyokuwa miaka kadhaa suala la Freemason. Ikawa kila mtu ni freemason. Mnaambiwa gari nyeusi ni za freemason. Nishawahi kimbiwa mimi sababu ya kuwa na gari nyeusi full tinted kwa upumbavu tu kama huu.

Miaka ya nyuma tulikuwa na Mumiani, wanyonya damu hawa nao walitusumbua sana . Ikawa ikionekana gari nyekundu basi ni ya mumiani, wanyonya damu...


Watanzania acheni upumbavu. Ishini maisha yenu. Fundisheni watoto wauchukie ushoga, wachukie tabia za koshoga na kisagaji. Wasikimbie rangi au upinde wa mvua. Acheni huo Ujinga.
 
tukalitazame na ili tokea kupata huru wanashinda kwa kishindo
 
namba ziache kushawishi kujiunga freemasons 0786762144 na 0765552597
 
namba hizi ziache kushawishi watu kujiunga freemasons 0765552597 na 0786762144
 
Back
Top Bottom