Tulieni - Kuna ubaya gani Raisi kujadiliana kupingana na wenzake ???

Tulieni - Kuna ubaya gani Raisi kujadiliana kupingana na wenzake ???

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Mbona watz mnakuwa watu msioeleweka kivile.
Yule mlimwita Baba Haambiliki ,Magufuli hasikilizi ushauri na sasa mkipata aliekubali kukoselewa ,nafikiri huwaga mara nyingi hugusia yupo tayari kukosolewa bado kwenu imekuwa shida,akitokea mtu kumkosoa au kwenda kinyume na Raisi mnapiga makelele na ghasia mujini,ivi mna akili timamu ?

Hebu ikubalini demokrasia katika ubora wake ,mtu mwenye uelewa kama mimi nikiwaona mnamsema Ndugai kwa kupingana na Raisi kimaelekezo ,mnachachamaa na hata upinzani nao wamepoteza dira ,ila kwa wapinzani sawa kisiasa mpinzani hatakiwi kusifu kitu au kusifia utawala ,liwe liwalo mara zote mpinzani anatakiwa awe opposite side kisiasa na si kiuhalisia.

Demokrasia sio lele mama mnapiga mayowe kutaka demokrasia izidishwe basi gharama yake ni viongozi ndani ya serikali kukokoromeana ni jambo la kawaida na lenye tija,kuliko kuona mtu anapotea mkamuachia kwa kuwa tu yumo ndani ya chama chetu au ndani ya serikali yetu ,sivyo hivyo Halafu likizama mnamtupia yeye ,wewe ulikuwepo wapi usimshauri au kumstopisha ?

Raisi Samia anaekukosoa,anaekufahamisha anae kuelekeza huyo ndie anaekupenda ,waogope wanaokusifia kwamba mfalme amevaa nguo nzuri.
 
Back
Top Bottom