Tulikotoka kufikia SADC sehemu ya tatu, Tanganyika na mkutano wa wapigania uhuru Kusini ya Sahara 1953

Tulikotoka kufikia SADC sehemu ya tatu, Tanganyika na mkutano wa wapigania uhuru Kusini ya Sahara 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TULIKOTOKA KUFIKIA SADC SEHEMU YA TATU

TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953
KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA WAPIGANIA UHURU WA KUSINI MWA SAHARA




1565496413824.png

Ally Sykes kulia na Denis Phombeah Uwanja wa Ndege wa Chileka, Blantyre Nyasaland wakirudishwa Dar es Salaam, Tanganyika baada ya kuzuiwa kuingia Lusaka, Northern Rhodesia

1565238184703.png

Ally na Phombeah waliwasili pale uwanja wa ndege mapema sana hata kabla milango haijafunguliwa.

Walitembea tembea kwenye jengo la uwanja wa ndege ambako walikuta vibanda vichache ambamo Waafrika walikuwa wakiuza chai na vitafunio.

Watu hao walikuwa wamesikia kuhusu mkasa wao pale uwanja wa ndege siku iliyopita.

Ally na Phombeah walipewa bure chai na vitafunio kupasha moto matumbo yao kwa kuwa hawakuwahi kuvunja na fedha.

Wale watu waliowakuta pale nje uwanja wa ndege walizungumza nao kwa upendo walipokuwa wakistaftahi wakiwaita ''comarades.''

Afisa wa Uhamiaji alirudisha pasi zao za kusafiria alizozichukua jana yake na akawauliza maswali machache ya kipumbavu ambayo Ally na Phombeah waliamua kutoyajibu.

Waliruhusiwa tu kupanda ndege iliyokuwa ikienda Lusaka baada tu ya Wazungu wote kupanda.
Ndani ya ndege waliambiwa kukaa nyuma mbali na abiria Wazungu.

Ally na Phombeah walikuwa ndio kwanza wanaanza kukaa kwenye viti vyao kama walivyoamuriwa mara afisa wa polisi Mzungu akaingia ndani ya ndege na kuwataka washuke na wamfuate hadi kwenye jengo la uwanja wa ndege.

Nje ya ndege wakaambiwa hawatasafiri kwenda Lusaka Northern Rhodesia isipokuwa Blantyre, Nyasaland. Ally Sykes na Denis Phombeah walilalamika na kupinga lakini walijibiwa kwa ufedhuli na kuamriwa kufunga midom yao.

Pale uwanja wa ndege wa Chileke Blantyre, wakanyang'anywa tean pasi zao.

Ilikuwa hapa ndipo sasa walitambua kuwa wamba kulikuwa na njama iliyopangwa vizuri kati ya zile serikali mbili za kikoloni kule Lusaka na Salisbury kuuvuruga ule mkutano wao wa vyama vya siasa Kusini ya Sahara.

Haya yaliyokuwa yamewafika yanaeleza ule ukweli wa jinsi wapigania uhuru hawa wawili walivyoonekana kuandamwa na kuwindwa kila mahali mamlaka za kikoloni zikipanga mipango yao bila tabu na kuwasababishia shida na usumbufu mkubwa.

Phombeah, ingawa alikuwa akifanya kazi na kuishi mjini Dar es Salaam, alikuwa vile vile vilevile familia na nyumba mjini Blantyre.

Phombeah alimkaribisha Ally nyumbani mwake huko mjini Blantyre na wakaanza kufanya mipango mipya ya ya namna ya kusafiri kwenda Lusaka kwa barabara na ili kuwahi mkutano.

Lakini kabla ya kuanza safari waliamua kutafuta ushauri wa kisheria ili kuzuia uwezekano wowote wa usumbufu toka mamlaka za kikoloni.

Ally na Phombeah walikwenda kumwona Henry Chipembere, ambaye alikuwa mwanasiasa wa kuheshimiwa miongoni mwa Waafrika mjini Blantyre.

Chipembere kwa busara aliwashauri wasitafute msaada wa kisheria dhidi ya serikali kwa sababu wangekuwa wakijiongozea matatizo wao wenyewe.

Kwa kuwa hawakukubali ushauri wake Chipembere aliwakutanisha na wakili mmoja ambae aliyewashauri kurudi nyumbani.

Baada ya kudhibitisha kwamba hakukuwa na njia yoyote wangeweza kwenda Lusaka kutokea Blantyre, Ally na Phombeah walimpelekea telegram Kaunda wakimjulisha yaliyowafika Salisbury.

Kaunda alijibu telegram yao siku ile ile akieleza masikitiko yake kwa yote yale yaliyousibu ujumbe wa Tanganyika.

Baada ya haya Ally na Phombeah waliandika barua kwa ANC, Rhodesia ya kaskazini wakiahidi mshikamano wa TAA na harakati katika nchi zote za kuikomboa Afrika kutoka ukoloni.

Kaunda alipokea kwa shukrani salamu za TAA na kahidi mshikamano ambao kwa kweli umedumu baina ya Zambia na Tanganyika hadi sasa.

Safari ya kurudi Dar es Salaam ndege nzima ilijaa Makaburu na Waafrika pekee waliyokuwa ndani ya ndege ile walikuwa Ally na Phombeah.

Ally na Phombeah hawakupewa vinywaji kama abiria wengine. Chakula na vinywaji vilitolewa kwa Wazungu tu.

Wakiwa ndani ya ndege ile baada ya mkasa wote ule mjini Salisbury na Blantyre, Ally aliwafikiria Waafrika waliokufa katika Vita Kuu vya Pili vya Dunia wakipigana chini ya bendera ya Uingereza.

Waafrika waliopigana kulinda dola ya Waingereza watu ambao sasa walikuwa wakiwatemea mate usoni.

Mkutano wa Lusaka ulihudhuriwa na wajumbe wachache sana. Wajumbe wote wa kutoka Afrika ambao walithibitsha kushiriki walishindwa kuhudhuria.

Waliothibitisha kuhudhuria mkutano ule walikuwa W. W. Awori kutoka Kenya, E. K. Mulira - Uganda, Masopera Gondwe - Nyasaland, Benjamini Borombo - Southern Rhodesia.

Borombo aliambiwa ni mhamiaje asiyetakiwa alipotia wake Northern Rhodesia.

Gondwe alinyimwa tiketi na kampuni moja ya mabasi, Thatcher Hobson Transporters. Baadaye Gondwe alitafutwa na askari kuhojiwa.

South African National Congress na South African Indian Congress zilimpelekea Kaunda taarifa ya pamoja kuwa kuwa kwa sababu ya matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wao yamewazuia kuhudhuria mkutano.

Abdulwahid, Nyerere, Dossa Aziz na Rupia walifika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kuupokea ujumbe wa TAA toka kwenye mkutano wa Lusaka ambao hawakuhudhuria.

Makao makuu ya TAA yalikuwa yakifuatilia matukio yale ya Southern Rhodesia kwa fadhaa kubwa.

Gazeti la Tanganyika Standard lilikuwa na haya ya kueleza:

''Reuter imearifu kwamba Itla Ung, mjumbe wa Burma katika Umoja wa Mataifa, amewasili Lusaka kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa Kusini ya Sahara, ambao unatafuta njia za kuimarisha harakati za kitaifa katika nchi husika za Afrika.

Wajumbe 14 kutoka Kenya, Uganda, Tanganyika, Zanzibar, Nyasaland na - Rhodesia zote mbili wamealikwa kuhudhuria mkutano huo uliyoitishwa na ANC ya Northern Rhodesia.

Hla Ung alisema aliwakilisha Asian Socialist Conference.

Wajumbe 8 waliotarajiwa kwa ndege siku ya Alhamisi walishindwa kuwasili.

Maofisa wa mkutano huo wa Rhodesia ya Kaskazini walisema wajumbe waliokosa kufika walikuwa wametuma telegramu wakisema wangehudhuria lakini hakuna maelezo yaliyotolewa kwa kutowasili kwao.

Mjumbe kutoka Southern Rhodesia alipigwa PI kama mhamiaji haramu asiyetakiwa na mamlaka za Rhodesiaya Kaskazini kule Livingstone kutokana na sababu ya hakuwa ya kutokidhi masharti.

TAA iliitisha mkutano wa viongozi wa chama na Ally na Phombeah waliwakilisha taarifa yao.

Baada ya kupokea taarifa hiyo,

TAA iliazimia kufungua mashitaka mahakamani dhidi ya serikali ya walowezi "kuipinga haki ya nchi kukatalia wasafiri kupitia humo nchini wakiwa njiani kwenda nchi nyingine, kuendelea na safari yao."

Serikali za kikoloni nchini Tanganyika, Kenya, Uganda, Nyasaland na Southern Rhodesia kwa kushirikiana walifaulu kwa njia moja au nyingine kuwazuia wajumbe wa Kiafrika kuhudhuria mkutano ule.

Hla Ung, mjumbe wa Burma kwenye Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Asian Socialist Conference, alikuwa peke yake ndiyo mjumbe peke yake kutoka nje aliyehudhuria mkutano ule.

Hla Ung alitoa hotuba iliyovutia sana ya mshikamano pamoja na watu wa Afrika.

Katika taarifa yake ya mkutano ule iliyotumwa kwa makatibu wa vyama vya siasa, Kaunda aliishutumu serikali ya Kiingereza kwa kuuzuia mkutano huo.

Ijapokuwa TAA haikuwakilishwa kwenye mkutano huo, urafiki na mshikamano baina ya Kaunda na wazalendo wa Tanganyika uliendelea.

Kaunda alikutana na Nyerere kwa mara ya kwanza miaka mitano baadaye mjini Dar es Salaam mwaka wa 1958.

Urafiki baina ya Kaunda na Nyerere na Tanzania na Zambia ambao haujatetereka inaweza ikasemwa kuwa asili yake ni ile safari ya mwaka wa 1953 ya Lusaka aliyofanya Ally Sykes na Denis Phombeah.

Mwisho
 
Tuliambiwa watakuja marais wengi na watu wengi kama elfu mbili na kumi na nne kwa ajili ya mkutano wa SADC na tukaambiwa tusiende bila kuoga mjini, vipi mkutano unaendeleaje huko?
 
Denis Phombeah mufti sijapatapo kuskia wala kusoma habar zake
Sijajua ni mm au ni kweli hukuwah kuandika chchte kumhusu yeye na mchango wake ktk Tanganyika
Km hutojali tafadhali tupe kidgo tawasifu yake na Taathira aloiacha ktk historia yetu ya Tanganyika/Tanzania
 
Denis Phombeah mufti sijapatapo kuskia wala kusoma habar zake
Sijajua ni mm au ni kweli hukuwah kuandika chchte kumhusu yeye na mchango wake ktk Tanganyika
Km hutojali tafadhali tupe kidgo tawasifu yake na Taathira aloiacha ktk historia yetu ya Tanganyika/Tanzania
Mwinchumu,
Huwezi kuamini hivi punde Francis Chirwa kanipigia simu.

Mimi sikuwa na taarifa kumbe gazeti lao Raia Mwema wamechapa makala
yangu kuhusu Denis Phombeah.

Sasa jamaa wa nyumbani Malawi kusoma hiyo stori wakawapigia simu kutaka
taarifa zaidi za ndugu yao.

Nakuwekea kitu hapo chini umsome Phombeah na mengine:

 
Mwinchumu,
Huwezi kuamini hivi punde Francis Chirwa kanipigia simu.

Mimi sikuwa na taarifa kumbe gazeti lao Raia Mwema wamechapa makala
yangu kuhusu Denis Phombeah.

Sasa jamaa wa nyumbani Malawi kusoma hiyo stori wakawapigia simu kutaka
taarifa zaidi za ndugu yao.

Nakuwekea kitu hapo chini umsome Phombeah na mengine:


Inshallah Mkuu
 
Back
Top Bottom