Tulikuwa tudogo

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
244
Reaction score
166
Hii aliwahi kunisimulia anko wangu ambaye ni mwanajeshi:
Ilikuwa ni wakati alipokuwa kwenye mafunzo ya afsa Kadeti kule Monduli. Mafunzo haya ni magumu sana kwani ndiyo yanayozalisha maafisa wa jeshi wa ngazi za juu kama vile Mabrigedia na majenerali wa Jeshi letu la wannchi yaani JWTZ.
Basi wakiwa katiaka mafunzo hayo siku moja waliamshwa alfajiri sana na siku hiyo ilinyesha mvua kubwa sana usiku na alfajiri hiyo bado kulikuwa na manyunyu madogo madogo.
Wakiwa na mkurufunzi wao wakaanza mazoezi ya kivita msituni, mazoezi mazito ajabu huku wakipigwa na baridi kali ya mwezi wa sita, lakini kutokana na ugumu wa mazoezi walikuwa wakitokwa na jasho.
Walipomaliza kipindi cha mazoezi hayo ya asubuhi, yule afande aliwapeleka katika eneo ambalo kulikuwa na kisima ambacho walikuwa wanatumia maji yake kwa kunywa au kuoga.
Kisima hicho kilichimbwa porini makusudi kwa ajili ya matumizi yao wakiwa kwenye mazoezi.
Walipofika wakakuta pembeni ya kile kisima kuna mavi ya binadamu ambayo yalikuwa yamezolewa na mvua na kuletwa pale kisimani na kwa jinsi palivyoonekana mavi mengine yalikuwa yameingia kisimani pia.
Yule afande akawaamrisha wakizunguke kila kisima, kisha akasema kwa amri kwamba akifumba na kufumbua asione yale mavi yaliyosambaa pale pembeni ya kisima.
Kama unavyojua kuwa katika jumuia yoyote hapakosi watu wabishi, basi wapo waliookota na wengine hawakuokota wakauchuna na kujifanya wameshika mavi kumbe walishika mchanga.
Basi yule afande akasema, kila mmoja apite mbele yake na kuonesha mavi aliyookota kabla ya kwenda kutupa na kama kuna mtu hana mavi mkononi mwake anarudi kwenye mazoezi upya na adhabu nyingine zitafuata.
He! kusikia hivyo wale waliozuga kwa kuokota mchanga badala ya mavi wakaanza kuwaomba wenzao mavi ili wasije wakapata adhabu ile.
Ilikuwa ni kasheshe kwani kila anaeombwa mavi alikuwa akikataa kata kata kwa kudai kwamba hana mavi ya kutosha.
Sasa kulikuwa na jamaa mmoja kutoka mkoani Mbeya, yeye alipoombwa mavi na mwenzie akapaza sauti na kumjibu mwenzie,
"He Mnyapala siwezi kukupa tu mavi twangu, kwani tu mavi twenyewe ni tudogo" Basi wenzake walicheka mpaka mbavu zikawauma.
Yule afande kusikia hivyo akauliza, "Aroo, ni nani huyo anaomba mavi ya mwenzake"
Jamaa akatatajwa, we! mbona moto ulimuwakia.

Kilichoniacha hoi kwenye kisa hiki ni kwamba, kumbe wakati mwingine mavi yanaweza kuwa na thamani kama almasi………..


 
HADITHI HII INATUFUNDISHA KUWA WATU WAONAOTOKEA Mbeya NI WABISHI TANGU ZAMA ZA KALE ZA MAWE.
KIKWETE KWELI KAZI ANAYO.
 
Wanakumbushia wahenga walisema;"One's man trash is another man's treasure!"...ila sikudhani treasure yenyewe ingekuwa mavi..duh!
 
Uvivu au kutegea kazi hakufai utaishia kuomba mavi ya wenzio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…