Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Tukiwa shule ya msingi, tulipewa eneo la kulima. Tuligawanywa maji si ya watu kumi na kila kundi lilipiga kura kumchagua kiongozi wa kundi. Amina alipata kura nyingi katika kundi letu hivyo akawa kiongozi wetu.
Tulipewa majembe na kuanza kuchimba mafuta. Kila kundi liliamua nini kitapandwa katika tuta lao. Wengine walipanda nyanya, Chinese, vitunguu, sisi tulipanda mchicha. Tulipewa mbegu na tuliotesha vitalu. Tulitaarisha matuta na mbolea na baada ya wiki mbili tulihamisha mchicha kwenye mafuta. Tulipewa ndoo za kumwagia bustani kabla ya kwenda nyumbani baada ya masomo.
Mchicha wetu ulifikia pa ki una, ulivunwa na kuuzwa kwa walimu. Kitu ninachokumbuka ni kutopewa mrejesho wa kazi yetu. Hakukua na taarifa ya mapato ya mchicha wetu. Ilipaswa tupewe mrejesho na kuambiwa katika pesa hizi mnaamua tununue nini? Ninadhani wengi tungeamua kula ice cream lakini huu ulikua mwanzo mzuri wa kufundishwa kilimo, kujitegemea na pia demokrasia.