Michael Ngusa
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 1,637
- 463
Majuzi mke wangu alisema mwanetu kafikisha umri wa kuanza kupewa vyakula laini na pia maziwa, asitegemee sana kifua chake. Basi mzee nikazama Nakumatt pale Pugu road, nikaelekezwa sehemu ya maziwa.
Lakini kwakweli sikuona maziwa ya mtoto, sana sana ni ya NIDO ambapo na yenyewe nilikuwa nashangaa mbona yana picha za vijana wakubwa na mama yao, nikasema anyway nisiangaike sana, nikalipia na kumfikishia wife nyumbani.
Siku ya pili nikasema hebu nionje huu unga unga, hawa watu wanayafanyeje maziwa ya ng'ombe yawe unga unga! nikachota kijiko na kuanza kulamba, kwakweli sikuacha, nimeendelea hivyo kila nikirudi kutoka kazini.
Mke wangu alikuwa anasema "wewe utamaliza maziwa ya mtoto!" mie namjibu aaah leo mwisho! najikuta tu naendelea hadi siku hii ya 4 kopo limeisha kabisa na mwanangu akiwa ametumia kama vijiko viwili vitatu tu.
Kusema kweli ni matamu ingawa najuta na nina wasiwasi hii tabia ya lambalamba inaninyemelea, hapa nipo njiani naelekea kumchukulia kopo lingine, nitajitahidi kwakweli zamu hii niuchune.