Heri ya Christmas.
Technic zangu ni zilezile, mademu chuo ninao wengi wa kuruka nao ila sidate na yeyote. Wiki ngapi hizi zimekuwa za vizinga vingi na kujichekesha na kunimiss, mara kuuliza nitaenda wapi, nitakuwa na nani.
Niko zangu maskani nimetulia kabisa. Sipendi kelele na fujo, viwanja leo vina wasumbufu ambao hawaendi hata bata ila leo wamejitutumua. Ukiingia malls ndio utashuhudia uchafu na usumbufu, beach ndio kabisa, swimming usiseme.
Sikukuu zikiisha January itakuja na njaa, viwanja vitabaki na legends, bumu limekata, baba zao ndio watakuwa wamelipa ada, nyodo hakuna tena. Mimi ultra legend ndio nitaingia kuplay party yangu. Mwaka jana nilifanya hivi na nilienjoy sana. Anayecheka mwishoni ndiye hucheka zaidi.
Bahati nzuri mimi sio shabiki wa sikukuu. Nikisali na kukesha imeisha nabaki na amani kuu.