sir mweli
JF-Expert Member
- Feb 8, 2017
- 495
- 573
Tuliosoma Pugu boyz kuanzia miaka ya 2000 kuja juu njooni tupigeni story, kwanza mi nauliza kila Mara nipitapo ile njia kuelekea Kajiungeni huwa hali yangu inabadilika. Huwa nahisi kama narudi gerezani. Kiufupi nahisi nime afectika kisaikolojia na ile life ya pale, sijui nyie wenzangu.
Tuachane na hilo, vipi wenzangu tuliokuwa pale miaka ya 2011 mnakumbuka mabomu ya Gongo la Mboto, mzee ilikuwa balaa, kuna jamaa alikuwa anamdaia mlemavu mmoja na ile wheelchair asa alipoona mabom yanazidi akamwacha akakimbia, kufika pondi anamkuta mlemavu kashafika saa nyingi [emoji23][emoji23][emoji23]
Acha hiyo, nyingine hii, hivi yule Mbagala alikuwaga na mota nini, asubuhi kanitoa nduki bwenini sijaenda assemble, kila nikigeuka huyu hapa, kila nikigeuka huyu hapa mwisho nafika Majoe ikabidi nisimame tu anikamate, cha ajabu mara akanipita heeh kumbe alikuwa anapiga zake zoezi.
Ila yote kwa yote Pugu imenifundisha laifu yaani ukitoka pale mahali popote unaishi, Kuna Ticha wangu huyo sitakaa nimsahau, Mwl. Rwezaura Mungu amlaze pema peponi amina, Yule mwalimu kiukweli Hesabu anajua, Yaani toka naaza fom 5 hadi namaliza 6 kakata topik zote bila kuingia hata na kipande cha karatasi, yeye anaingia na chaki tuu, na anakata madude mengine hata Mchikichini hakuna aliyewahi kuyagusa. Na humpi swali akachemka, wala hakufanyii anakupa njia paka unajiona mjinga.
Nakumbuka mengi sana. Ebu na nyie wadau tupeni ya shuleni kwenu kidogo.