Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Binafsi nimewahi kutembea umbali takribani kilometer 100.

Ilikuwa ni safari ya kwenda na kurudi na ilinigharimu siku moja ya kwenda na siku ya pili ya kurudi.

ilikuwa nimeelekea msibani na nilikuwa na nauli ya kwenda tu, kwa sababu nikapata company ya mtu ambaye hakuwa hata na hiyo ya kwenda tukaungana na kuanza kupasua pori mdogo mdogo.

Safari ilihusisha kupanda na kushuka milima, mvua ilinyesha na kukatika karibu mara nne ila hatukukata tamaa.

Ninajua watu wametembea kwa miguu umbali mrefu kwa sababu nyingi zikiwemo:
kukoswa nauli
kutafuta kazi
Kuepuka hatari
hakuna namna ya kusafiri
na sababu nyingine nyingi ...

karibu utujuze
 
Kuna siku nilienda kumsalimia bibi . Wakati wa kwenda nilipanda gari, nilishuka kituoni nikatembea kuanzia saa 9alasiri hadi saa 12 na nusu jioni(Sijui ni km ngapi)
Kesho yake tukaondoka saa 12 nasu asubuhi tukafika saa 4 asubuhi
Pia kuna siku nilitembea kutoka mnazi mmoja hadi ukonga banana. Ilikuwa 1987
 
Mshuza2,
Kweli, ila hawa walitoroka gerezani huko siberia.

Wazungu wengi wanavision za ajabu, unaweza kukutana hata na mzungu anavision ya kuzunguka dunia kwa miguu.
 
O levo nlkosaa nauli likizo ya mwez wa 6. Nlipga kwata kilometers 30 . Alafu dem wangu wa shule s akaniona wao walikuwaa na rafk zake ndan ya bas aseee alivonipungia mkono na kunitajaa jna nlitaman kulia .Maisha haya nyie achen tu .YOTE HAYA NLKULA NAULI
 
Back
Top Bottom