Tuliowahi kuibiwa vitu majumbani, kwenye gari, n.k -- ni kitu gani hukudhania wangeiba?

Tuliowahi kuibiwa vitu majumbani, kwenye gari, n.k -- ni kitu gani hukudhania wangeiba?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Binafsi nakumbuka nikiwa chuoni Arusha, kuna siku nlikuwa nahamia geto flani.

Basi tripu ya kwanza nilipeleka mapazia, meza na kitanda.

Sasa wakati nimemaliza kufunga kitanda nimechoka hatari, nikanunua bia mbili, kwajili ya mimi na jamaa kanisaidia kufunga kitanda, tulipiga pafu moja tu, kirikuu ikaja tuchukue vitu vingine, tukazifunga safari zetu na vizibo.

Wakati narudi mida ya jioni nikakuta kitasa kama kimepinda, kumbe wezi waliingia aisee!

Walibeba viti viwili na pazia, kilichonita zaidi zile bia waliinywea pale pale wakaiacha chupa tupu, bora wangeziacha nitoe stress za kuibiwa, ule haukuwa uungwana.
 
Pole sana mkuu.

Walimwagilia mioyo yao pale pale kujipongeza kwa mission yao
Screenshot_20220526-102632~2.png
Mnyampaa habari ya mpindi
 
mwiko wa ugali aise wale wezi wajinga sana.
 
wezi wengine walikula wali kiporo pumbav sana wale.
 
Mimi waliingia kwenye friji wakanywa coca wakaacha nyagi paba mbili ila msala pale mlangoni walikata magogo vifungu fungu
 
Kuna day tupo Mlalakuwa( Mwenge Daslam) tunasoma chuo tulishazoea kutofunga mlango tunarudishia tu na tupo mtu tatu. Tulikuja safishwa laptop 4, smartphone 3 na kitòchi, baku baku zenye kimango shente. Asee tuliumbuka sana hata ndugu hawakutulewa maana tulikuwa mawaki sana tulijisahau kumbe wanatusomea gap.
 
Back
Top Bottom