Tuliowahi kukaa muda mrefu bila kulala uzi huu hapa

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,508
Reaction score
2,619
Salaam kwenu!

Ulishawahi kukaa muda gani (siku ngapi) bila kulala? Kwa nini.

Binafsi sitosahau tulikuwa tunahama na mifugo, ndo mara ya kwanza kuingia kwenye misafara hyo (baada ya kumaliza shule).

Siku ya kwanza tulitoka Ifakara mida ya saa mbili usiku hadi kesho yake jioni tukafika Mang'ula. Hapo tukakaa kidogo, hadi mida ya saa nne usiku tukaliamsha (kumbuka hapo kukaa kidogo si kwamba unalala, NO) yaani unachunga mifugo ikitulia unaegemea mti kidogo. Dah, hakuna siku nilichoka na kushikwa na usingizi kama hiyo maana tulipita barabara inayopita kati kati ya shamba la Miwa la Kilombero. Dooh, lile shamba kubwa jamani. Nakumbuka tulianza safari hyo saa nne had 11 alfajiri tukafika Msolwa.

Mchana ule tulizurura Msolwa (bila kulala) hadi saa 11 jioni tulivyovuka mto Ruaha kuingia Selous.

Yaliyotukuta Selous sisemi. Halafu ilikuwa ni mwendo wa siku 4 hadi Kisaki (yaani hakuna maji, hakuna watu useme utaenda kuomba maji wala nini).
 
sitasahau popobawa alivyokuwa anapitia watu nakumbuka nilikesha zaidi ya siku 365 na nusu kumuogopa popobawa.mchana napiga kazi kawaida usiku nachanja gomba jumlisha kunywa na kahawa kuogopa adha ya popobawa.

usingizi ukizidi sana naweka miguu kwenye beseni lilojaa maji...mpaka stori za popo zilivypotea ndo nikaacha kukesha tena ndani ya wiki mbili baadae ndo nikapata usingizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…