Aise siwezi kusahau ilikuwa mwaka 2010 nikiwa nipo sekondari kuna mzee alikuwa na kawaida ya kutongoza wavulana siku hiyo akaniita akamwaga sera zake kilichofuata baada ya hapo nikampa majibu ya hovyo ambayo yalimuuma na rafiki zangu wakaja nao wakampa matusi ya kutosha,baada ya siku mbili mzee akaenda kushitaki kituoni kwamba sie ni wezi tukaja kukamatwa usiku mida ya saa nane tukiwa tumelala mlango ukagongwa tulifungua tukafungwa mashati na pingu mikononi mpaka kituo cha polisi mpaka asubuhi,tulikamatwa wanne tena wawili tulikuwa wanafunzi,wengine wawili walikuwa saidia fundi garage, asubuhi ikaja kuripotiwa kwamba watoto wamepotea pale kituoni ikabidi afande aulize "ndio yale majambazi tuliyokamata usiku?"cha kushukuru sura zetu na wizi haziendani maana hata bangi wala pombe hatukuwahi kutumia ikabidi afande aelezwe full story A to Z ndio tukaachiwa tena free bila kutoa hata senti,hiyo ndio ilikuwa siku niliyolala selo japo katika maisha yangu nilishajiwekea siku za nyuma kwamba siwezi lala selo mimi,siwezi kusahau aisee