Bombabomba
JF-Expert Member
- Dec 23, 2017
- 1,804
- 2,128
Nimekumbuka mbali sana.
1. Niliwahi kupigwa na mbabe mmoja huko kijijni kwetu tukichunga mbuzi. Yeye kazi yake ilikuwa kutuma wenzake tu hadi anaboa. Beberu wake akipigwa na wako naye anakupiga. One day nikamkatalia manyanyaso yake akaanza kunipiga, nikawaambia jamaa tupigane, jamaa wakashika mchanga sote tukapuma kukubali kupigana.
Kwa vile yeye tayari mbabe, akanijia kasi mimi nikawahi miguu nikamlalia, nikampa kichapo hadi damu puani na mdomoni. Akaomba msamaha tukaamuliwa. Then kutumana kukaisha.
2. Nikiwa darasa la pili kuna mbabe kiongozi wetu aliniaibisha mstarini kaniambia nina chawa mgongoni. (Tuliosoma 1980-90s chawa na funza ilikuwa ni kitu cha kawaida sana, hasa vijijini)
Akiwa amejisahau nilimshambulia kwa jiwe moja tu - tunayopanga mstarini hadi alilia, nikaishia kushambuliwa na wababe wengine na walimu na kuandikwa black book.
3. Nikiwa darasa la tatu, kuna mbabe wetu class nilimtania ameota nywele matakoni (mwenzetu alikuwa mkubwa kama 14-16 hivi, sisi tukiwa 11-13, hatukuwa nazo), niliziona tulipoenda oneshana vyupi VIP!
Jamaa alinipiga na kuninyanyasa daily, siku hiyo wakati ameniita ili anipe manyanyaso nikamtemea mate usoni, akijifuta nikamuunganishia ngumi mfululizo akiwa kakaaa dawatini, mimi nipo free huku nikishangiliwa hadi ticha akaja kuamua. Nikapigwa bakora assemble na kuandikwa black book mara ya 2.
Jamaa baadae aliacha shule darasa la nne tukiwa tunaheshimiana. Mwishowe hiyo black book ilipotea ofisini kwa Mkuu wa Shule. Tulishukuru kwa kuwa kilitisha sana.
4. Sekondari nilipigwa katika ubabe wa shule jirani, lakini pia kwenye kufukuzia mademu, kaka zake walinitandika hadi nikashindwa kukimbia. Demu nilimkosa japo sasa kachoka tayari.
5. Nilipigwa na polisi nikizamia uwanjani kucheki mechi ya Yanga hadi nikapoteza fahamu kwa muda; nikastukia napepewa na wasamaria.
Nafurahi kwa sasa sina adui yeyote katika maisha yangu na sipendi ugomvi kabisa. Hata home na wife tuna zaidi ya 15 yrs hatujawahi pigana.
Nawe tukumbushe kile kichapo unachokumbuka hadi sasa.
Sent using Jamii Forums mobile app