Kuna jamaa miaka ya nyuma alikuwa kibaka, saizi kaokoka kaachana kabisa na mambo hayo. Sasa kwakua ni mtu mwenye interest na mchezo wa draft sikumoja tukamuuliza ilikuwaje kuwaje mpaka ukaachana na ukibaka
Akatuambia kua alikuwa na crew ya vibopa wawili, nayeye jumla watatu. Jamaa ndio alikua kiongozi wa hilo gang ambapo majukumu yake yalikua ni kupiga kabali halafu wale wawili kazi yao ni kuja kusachi mifukoni
Sasa unaambiwa mchizi alikuwa ana style yake ya kupiga kabali ambayo akisha kuleta kwenye kifua chake hauchomoki, na wale vibaka wawili wanakua wanajua tu tayari pale kabali imekubali ni muda sasa wasisi kwenda kusachi
Kuna siku moja walimuona jamaa akitoka benki na kile ki-briefcase afu kaulamba suti, vibopa wawa wanamlia timing, mara yule mdingi akasimamisha daladala na wao wakajipakia humo humo
Jamaa akashuka nao wakashuka na kuanza kumfata mdogomdogo kwa nyuma kwa machale zaidi ili wasistukiwe. Basi yule faza akaiacha main road na kuingia chocho, vibaka wakasema yees
Vibaka walipoona eneo hilo halina mpishano wa watu na kuhakikisha hakuna mtu mwingine zaidi yao na yule faza wakaamua sasa kufanya mpango wa kumpora bag yule mdingi
Ikabidi sasa wale wawili wajifiche sehemu afu atangulie master mzee wa roba ili hawa wengine wakishaona roba imekubali wasogee kupora lile begi
Basi master akanyata kwa nyuma na alipomkaribia yule mdingi akapitisha mkono shingoni kilichotokea yule dingi ule mkono ambao ulipitishwa shingoni mwake na yule kibaka aliyesimama nyuma yake, mdingi akaubana ule mkono wa yule kibaka uliopita shingoni kwa kidevu, huku mkono wake mmoja ukiwa mfukoni na mmoja ukiwa umeshikilia lile bag
Hawa vibaka wawili wakawa sasa wanaskilizia roba ikubali ili wasogee, lakini kila wakiangalia mazingira wanaona mambo yamekuwa magumu kwa mwenzao, walichokua wanakishuhudia ni jitihada za mwenzao kuhangaika kutoa ule mkono uliobanwa na kidevu cha yule dingi.
Alichokifanya yule dingi akautoa ule mkono ambao aliuweka mfukoni kisha akaunyoosha juu akauzungusha kwa nyuma akakamata shati pamoja na nyama ya bega afu akamnyanyua juu akamtua mbele yake kibaka akasikika akisema "samahani braza nilikua natania" afu mdingi akamshushia kikombe cha maana wacha aagawe ile kuamka kibaka kasepa na njia
Kumbe kibaka aliingia kwenye zone ya komando