Tuliowahi kushikwa na tumbo la kuhara kwenye mazingira hatarishi tukutane hapa

Tuliowahi kushikwa na tumbo la kuhara kwenye mazingira hatarishi tukutane hapa

IMG-20240117-WA0583.jpg
 
Huu uzi unanikumbusha mbali sana,ilikuwa mbeya to dar nishashindilia kiporo Cha wali harage asbuhi nlichokosea nlichoma ndumu kabla sijaondoka,Basi kufika stendi nkapangwa siti na mtoto mzuri,hapo sikohoi sijambi Kila nikitaka achilia bomu la nyuklia nawazia mtoto mzuri pembeni,basi tumbo likaanza unguruma kama Lina mota,na mbaya zaidi Kwa nguvu Hadi manzi akawa anastuka.Hapo nusu ya safari Bado siongei najikaza jasho ndio lanitoka kwamba nikiachia tu natawanya basi Zima basi,Mungu saidia tukawa tumeingia hoteli kuchimba dawa nilipofika nikiachia kitu watu nje walistuka kinoma maana walizani bomu la mkono.
Funzo: ukitaka kujamba we Jamba usirudishe ndani ni hatariii
 
Daaah kuna siku nasafiri dar bukoba gari ilifeli ruvu tu hapo tumetoka kwa kuchelewa Mohamed Trans hyo Gairo saa kumi na kama saa nane hivi tumeshuka kula nikala yale ma egg chop ndo yalikua mengi ebana kufika dom mbele mbele hiv tumbo limechanganya nkaenda kwa dereva na wenzie pale kuwaeleza shida yng wakanambia angalia nje hakuna kichaka utajisaidia wap na hapa nikipaki gari abiria watashuka ko vumilia had Manyoni ebana sio poa... Kufika manyoni nkaelekezwa pharmacy nikaingia nalipa tu naskia mzigo unataka kutoka nkazunguka nyuma choo cha kulipia mchukua hela kalala nikaingia shusha mzigo pale natoka bado kalala nkasepa nkapitia dawa nikanywa nikatulia ile siwez isahau.
 
Nakumbuka nilikuwa natoka Arusha - Mwanza miaka hiyo 2015. Mapema asubuhi tumewahi pale stand kuu arusha na rafiki yangu yeye alikuwa anaelekea Dsm. Saa kumi na mbili kasorobo niko kwenye siti yangu ya mbele kabisa (nyuma ya dereva). Ilipofika saa kumi na mbili kasoro kama dakika tano basi linaanza kusogea nikasikia tumbo limekata chini ya kitovu. Nilidhani ni hali ya kawaida nikatulia tuli kisikilizia ile hali huku basi likianza kuondoka taratibu. Hali ikaendelea kuwa mbaya nasikia nataka kuharisha nikajikaza huku kijasho chembamba kikinitoka. Nilivumilia sana lakini niliona kabisa abiria wa jirani yangu wamehisi siko sawa kwa nilikuwa najinyonganyonga mara nimeinama kulalia tumbo na maeneo hayo bado ni mjini huwezi kushuka kuchimba dawa. Baada ya kupata uwanja wa ndege kisongo angalao niliona mapori nikamshtua konda anishushe nikajisaidie vichakani. Hapo ni kama saa kumi na mbili kama na dakika 45 nimevumilia. Konda akanitupia chupa ya maji nikatoka spidi mpaka kwenye vichaka niliharisha mpaka nikaishiwa nguvu. Baadae nikarudi kwenye basi nikiwa mwepesi lakini kwa aibu kubwa (kijana mtanashati unakunyakunya maporini). Nilidhani shida imeisha baada ya kama dakika 20 ile hali ikarudi tena nikamuambia konda tafuta sehemu yenye kamji nishuke safari nitaendelea kesho, nikatoa begi langu nikawa tayari kushuka nashangaa abiria wa jirani yangu ananiuliza sasa nauli yako si itapotea nikamuambia kwa hali niliyonayo acha tu nishuke. Kufika sehemu wakanishusha wakaniambia hapo naweza kupata msaada zaidi. Baada ya kushuka nikakuta kumne wamenishusha Makuyuni. Nikashangaa shangaa pale nikaona jamaa wanauza vibanda vya bidhaa za watalii (curio shops) nikapiga nao story wakaniambia choo kiko kwa nyuma nikaingia nikakuta vyoo cha kisasa sana (nadhani ni kwa ajili ya watalii). Nikamaliza haja zangu nikarudi nikauliza kama kuna duka la dawa bahati lilikuwepo nikauliza dawa za kukata tumbo la kuharisha nikanywa baada ya kama lisaa limoja nikajisikia niko poa kabisa. Kwenye majira ya saa nne nikapanda Tata ya Arusha Singida...

Hii safari ya Tata mpaka Singida nikapanda basi la KVC la kutoka Dar-Mwz ni story nyingine ambayo inatakiwa kutungiwa kitabu. Ilikiwa na mabalaa.
 
Kikubwa kama unasafiri safari ndefu ya masaa mengi jitahidi usile vyakula vyenye michuzi au maji mengi watu hukatisha safari kutokana na kupata mshtuko wa tumbo.
OMBA SANA HII HALI ISIKUKUTE NJIANI UKO SAFARINI NA HAKUNA PA KUSHUKA KIJISAIDIA.
 
Hii ilimtokea ndugu yangu mmoja, alikuwa anatoka Tarime-Mwanza. Akafakamia chakula asbh plus maziwa mgando, sasa kufika katikati ya safari tumbo likaanza kumsumbua mara kuendesha kumepiga hodi, si akaogopa kumwambia konda akachimbe dawa, ( alikuwa hajui kiswahili enzi hizo) ikabidi ajimalize kwenye suruali, mara paap mzigo unashuka chini, ikabidi achukue kamba za viatu afunge suruali chini kwenye miguu mzigo usishuke.
Mda kidogo harufu ikaanza kuenea kwenye gari abiria wakaanza kulalama, jirani yake akamshitukia akamtaja, yaani alishushwa kwenye gari kama Yona alivyotoswa baharini.
 
😂😂 Dah, nimecheka sana kama mjinga. Japokuwa ni story ya kutunga
 
Hii ilimtokea ndugu yangu mmoja, alikuwa anatoka Tarime-Mwanza. Akafakamia chakula asbh plus maziwa mgando, sasa kufika katikati ya safari tumbo likaanza kumsumbua mara kuendesha kumepiga hodi, si akaogopa kumwambia konda akachimbe dawa, ( alikuwa hajui kiswahili enzi hizo) ikabidi ajimalize kwenye suruali, mara paap mzigo unashuka chini, ikabidi achukue kamba za viatu afunge suruali chini kwenye miguu mzigo usishuke.
Mda kidogo harufu ikaanza kuenea kwenye gari abiria wakaanza kulalama, jirani yake akamshitukia akamtaja, yaani alishushwa kwenye gari kama Yona alivyotoswa baharini.
Mkuu ,na sisi watu wazima tunapita hapa jaribu kutuheshimu mkuu Wang 😃😃
 
Back
Top Bottom