sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Mwezi November 2017 sitakuja kusahau, kuna siku nliamka nikajikuta kama nmekatwa na wembe hivi kwenye mkono , nikagundua kuna washenzi wamefanya yao usiku, nliogopa,basi hio siku nliomba na kusoma biblia kabla siku nzima
Ile nimeingia kitandani najifunika blanketi, naskia "cshaaaaaaaa" mchanga unamwagwa kwenye dali, Duh, nikaanza kukemea, omba omba omba, hadi saa nae usiku, nikaacha nyimbo za gospel zinakita usiku kuacha, nmeamka najichunguza nakuta chale mpya kifuani.
Dah nlikosa amani, nikapewa first aid nijipake chumvi na limao sehemu walizochanja na nichome mmavi mavi kabla sijalala, ila wapi.
,kabla sijalala nimeomba naingia kitandani naskia ngoma bwana, ndo ndi ndo buu huu ndu ndu. Ahhh nikasema kumekucha, nikabaki macho hadi SAA kumi baperuzi internet nikalala, naamlka nakuta kachale shingoni...dahhh hofu nliyopata acha tu.
Basi aisee ikabidi niende tu kwa chifu flani ivi anisaidie maana hawa wanaobandika vibao kwenye mistimu matapeli tu, nimeenda huko kwa chifu sikumkuta nikawakuta wengine ndugu na watoto wake.
Nikawaeleza tatizo na kuwaonyesha alama wakasema hio ni michezo ya yangu zamani za kale na wala hakikua kitu kipya kwao na kinatatulika.
Nikaelekezwa pa kwenda basi nikaenda huko, cha ajabu nilifikiria kwa mtaalam kutakuwa kama kwa karumazila yani kuna mafuvu, mikia, mapembe, n.k ila nlichofikiria sicho, nmeenda sehemu huko nikafika nikaeleza shida yangu, tukaenda kuchimba mzizi sijui kwa mti gani nikaambiwa nikifika niutwange niogee, nlichajiwa elf 5 nikaondoka.
Nlipofika tu home nikasaga fasta nikatwanga, nikapasha mashi nikatia humo, basi ndio mpaka leo sijakutana na kero zilizonisumbua kama kuchanjwa, kumwagiwa mchanga dalini ama kupigwa ngoma.
Ni hayo tu kwa upande Wangu, na bado naenda kanisani.
EDIT SITAPOKEA PM, CHA KUFANYA TAFUTA CHIFU UTAPEWA PA KWENDA, USIJE KUTHUBUTU KWENDA KWA HAWA WANAOBANDIKA MATANGAZO YAO KWENYE MISTIMU, UTALIWA