Polisi waliofika Jamii Media wame confiscate nyaraka za usajili wa BRELA and there is a compelling reason for that.
Labda tusome kwanza regulation iliyomkamata Maxence Melo:
Electronic and Postal Communications Regulation, 2011, Section 10 (1)
Any public or business entity in Tanzania shall register and use domains with country’s cc TLD, the dot-tz.
Key words hapo ni nini, "any entity in Tanzania..."
Kwa chombo ama huduma ya kimawasiliano ya kimataifa, nini kinakufanya uwe "any entity in Tanzania...," kwamba unasomeka na kuchangiwa mabandiko kutoka Tanzania? Au kwamba kuna mfanyakazi wenu au Mkurugenzi Mkuu ni Mhaya wa Tanzania?
Facebook, Instagram mitandao mingine ya kimataifa inapatikana Tanzania lakini hawajasajiliwa BRELA, mashine zao haziko Tanzania, kama JF, na hivyo sio any entity in Tanzania, hivyo hawapo chini ya kanuni za TCRA za kusajili country code TLD ya .co.tz.
Nyaraka za usajili wa BRELA ndio ushahidi muhimu wa serikali utakaotolewa mahakamani kama the only jurisdictional connection kati ya JF na Tanzania, na kuwalazimisha wafuate sheria za kielektroniki za TCRA. Na hiyo jurisdiction, unfortunately, tumewapa sisi wenyewe, hakukuwa na haja ya kujisajili.
Jamii Media ni mtandao wa kimataifa unaopatikana, among other countries, Tanzania. Jamii Media wanatakiwa wajitoe BRELA, operations zao, servers zao, kama ilivyo Instagram, hazipo Tanzania.