Tuliporuhusu sera ya 50 kwa 50 dhidi ya wanawake tulikosea

Tuliporuhusu sera ya 50 kwa 50 dhidi ya wanawake tulikosea

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Katika Sera mbovu Viongozi walizokosea, ni hii Sera ya 50 kwa 50!

Mtakumbuka mwanzoni mwa miaka ya tisini na mapema miaka ya 2000; Sera ya elimu ilianza kuwabeba wanawake kwenye ufaulu!

Wanawake waliopata madaraja ya chini ya ufaulu (lower division), walipewa kipaumbele cha kuchaguliwa kuendelea na masomo ya juu kama upendeleo ukilinganisha na wanaume!

Matokeo
Matunda yalianza kuonekana katika utawala wa Mkapa baada ya nafasi nyingi za ajira kuanza kupewa wanawake!

Lakini tafti nyingi zimefanywa na kuonyesha kuwa wanawake wengi waliopewa fursa zimegeuka kichomi katika ustawi wa jamii kutokana na familia nyingi kusambaratika!

Pili; utafiti unaonyesha mwanaume aliye oa mwanamke aliyeajiliwa huishi na mke huyo kwa mvutano mkubwa jambo ambalo huchangia hata mauaji kwenye baadhi ya wanandoa.

Tatu; Utafiti unadhihirisha kwamba, kadri mwanaume anavyopata pesa huwaza kumfurahisha mwanamke zaidi kuliko ambavyo mwanamke apatapo pesa huwaza kuishi mwenyewe mbali na mwanaume!

Hivyo ni bora zaidi kuwapa nafasi vijana wa kiume ili waweze kulea wake zao kuliko kuwapa nafasi wanawake ambao mipango yao ni kujitenga na waume zao wanapopata pesa!

Hata YESU Alipokuwa anateuwa mitume, aliteuwa Wanaume ili wanawake wabaki kuwa wasaidizi!

Bomu la haki sawa kwa wanawake ni Kansa ya kujitakia itakayotafna kizazi hadi kizazi!
 
Kweli kabisa usawa ni kitu ambacho napinga sana dunia imeharibika na inaenda kuharibika zaidi kwa sababu ya hii kitu.

Malezi ya single parent yanayotokana na sababu ulizotaja yanaenda kutuletea binadamu ambao ni tatizo kwenye jamii na tunaenda kuwa watu aina hii kwa wingi kabisa mambo yatakuwa hovyo Sana hapo baadae.

Kutaka usawa ni kukosoa uumbaji wa Mungu kuona mungu alifanya makosa kutuumba hivyo.
 
Kabsa, mwanaume atakula kwa jasho, mwanamke atazaa kwa uchungu!
Sasa kuzaa kwa uchungu hawataki wanataka kazi wafanye wao!
 
Mambo mengi yangekuwa yanafanywa na wanawake Taifa na Dunia kwa ujumla ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo ktk nyanja mbalimbali kuliko hali ilivyo sasa.

Wanawake wamepewa uwezo wa tofauti na Mungu wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yakafanyika kwa ufanisi mkubwa!

Wanawake bado hawajajitambua sababu wamekuwa wakozongwa na mfumo dume ambao umekuwa ukirithishwa kizazi hata kizazi!

Fikiria hata sasa Eti kuna makabila watoto wa kike hawarithishwi mali matharani ardhi?!
 
Swala la kujitambua mwanamke pamoja na kufanikiwa kiuchumi n.k halipaswi kuchanganywa na ukosefu wa nidhamu ya mwanamke kwa mumewe pamoja na familia.

Mwanamke anayejitambua aliyepata malezi na makuzi yenye misingi myema ikiwepo misingi ya Imani hapaswi kumdharau mume wake au kumfanyia ukorofi.

Vinginevyo iwe Mwanaume ndiye aliyeanzisha ukorofi ndani ya nyumba na kwa hiyo mwanamke anakuwa amechoka.
 
Mbona wanawake ambao ni maamuma wakorofi pia wapo wengi tu kwenye jamii?

Unashangaa mpaka unajiuliza Huyu mwanamke jeuri yake inatokanaka na nini?

Wanaitwa maskini jeuri!

Yani mtu yatima halafu anadeka hebu fikiria!

Kwa kusema hayo ni kuwa tabia ya kiburi, ujeuri, ukorofi, dharau n.k ya mwanamke haitokani na elimu au mafanikio ya kiuchumi bali ni matokeo ya mambo mengi ikiwepo tamaduni, Imani , malezi na makuzi n.k
 
Mkuu dmkali 50 kwa 50 ya kweli inaanza na matumizi ya ndani. Kama budget ya siku ni 20,000/= basi mama anatoa 10,000/= na baba anamalizia 10,000/= yake mbali na hapo ni siasa tu.
 
Mambo mengi yangekuwa yanafanywa na wanawake Taifa na Dunia kwa ujumla ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo ktk nyanja mbalimbali kuliko hali ilivyo sasa.

Wanawake wamepewa uwezo wa tofauti na Mungu wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yakafanyika kwa ufanisi mkubwa!

Wanawake bado hawajajitambua sababu wamekuwa wakozongwa na mfumo dume ambao umekuwa ukirithishwa kizazi hata kizazi!

Fikiria hata sasa Eti kuna makabila watoto wa kike hawarithishwi mali matharani ardhi?!
Uwezo wao ni katika malezi tu si kuwa kichwa (wanapokuwa na Mali kuongoza hubadilika )
 
Mwanaume amegizwa kuishi na mkewe kwa akili!

Wala siyo pesa wala mabavu!

Though pesa ni jawabu la mambo yote!

Muombeni Mungu awape akili za kuishi na wanawake zenu.
 
Unakuta Mwanaume anashindwa kumuelewa mkewe hadi anamuuliza “hivi wewe mwanamke unataka nikufanyie nini ili uache kunisumbua?”

Maana pesa nakupa unapotaka, shida zako nazitimiza, kwenu wakiwa na shida nawasaidia. Ada za Shule za watoto nalipa, n.k

Kumbe mume mwema ni zaidi ya hayo [emoji108][emoji108]
 
Mambo mengi yangekuwa yanafanywa na wanawake Taifa na Dunia kwa ujumla ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo ktk nyanja mbalimbali kuliko hali ilivyo sasa.

Wanawake wamepewa uwezo wa tofauti na Mungu wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yakafanyika kwa ufanisi mkubwa!

Wanawake bado hawajajitambua sababu wamekuwa wakozongwa na mfumo dume ambao umekuwa ukirithishwa kizazi hata kizazi!

Fikiria hata sasa Eti kuna makabila watoto wa kike hawarithishwi mali matharani ardhi?!
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapa!?
 
Hata Muzungu, Muhindi, Mwarabu, Mchina wanabagua mtu mweusi Mwafrika mwanaume wanatoa sababu hizo hizo ulizotoa, Mwanaume Mwafrika kama wewe haukuruhusiwa kuishi na Muzungu, Mwarabu au Muhindi sababu zao ni kama hizo ulizotoa, hata Utumwa Muzungu alisema imeandikwa kwenye Biblia kwamba Mwanaume mweusi kama wewe siyo Binadamu kamili na ulizaliwa kuwa Mtumwa, Waarabu wanaamini hivyo pia kwamba wewe ulizaliwa kuwa mtumwa mpaka aleo hii ukienda Mauritania hata Sudani Waafrika wanaume kama wewe wanauzwa utumwa na wanatumia hivyo hivyo vitabu vya dini.

Hivyo kama unafikiri Wanawake hawastahili haki sawa basi hata wewe Mwanaume wa Kiafrika unastahili kubaguliwa na kutengwa na Muzungu au Muhindi pia, ...
 
Hata Muzungu, Muhindi, Mwarabu, Mchina wanabagua mtu mweusi Mwafrika mwanaume wanatoa sababu hizo hizo ulizotoa, Mwanaume Mwafrika kama wewe haukuruhusiwa kuishi na Muzungu, Mwarabu au Muhindi sababu zao ni kama hizo ulizotoa, hata Utumwa Muzungu alisema imeandikwa kwenye Biblia kwamba Mwanaume mweusi kama wewe siyo Binadamu kamili na ulizaliwa kuwa Mtumwa, Waarabu wanaamini hivyo pia kwamba wewe ulizaliwa kuwa mtumwa mpaka aleo hii ukienda Mauritania hata Sudani Waafrika wanaume kama wewe wanauzwa utumwa na wanatumia hivyo hivyo vitabu vya dini.

Hivyo kama unafikiri Wanawake hwastahili haki sawa basi hata wewe Mwanaume wa Kiafrika unastahili kubaguliwa na kutengwa na Muzungu au Muhindi pia, ...
Ulichoandika hakuna kichwa wa miguu! Bibilia imeandika mwanamke atazaa kwa uchungu, na mwanaume atakula kwa jasho!
Sasa unapowapa nafasi za ajira Kazi ya jasho wanawake wengi maanake wanachukua nafasi za wanaume! Na kukiuka miiko ya Muumba, hapo ndipo shetani anamvaa mwanamke hakamatiki
 
Back
Top Bottom