Mtu wa kati
Member
- Jul 16, 2022
- 5
- 4
Kama taifa huru muumba wetu alikiunda kipande hiki,kama sehemu tu ya dunia yetu nzuri.
Taifa hili tukufu linaaminika kuwa ni makazi ya mwanzo ya binadamu wa kale,mabaki ya watu wa kale yaliyopo Olduvai Gorge Arusha, uwepo wa mbuga za Serengeti na Ngorongoro na uwepo wa viumbe vinavyopatikana hapa kwetu tu, yanasadifu yaliyopo miongoni mwa dhana za wanasayansi juu ya kuwa hapa ni makao ya mwanzo ya binadamu na ndipo maisha yalipoanzia.
TULIPOTOKA
Babu zetu walikuwa ni wajima wakiishi maisha ya kijima,maisha ambayo binadamu wote walikuwa sawa. Ugunduzi wa kisayansi na kukuwa kwa Teknolojia kuliwafanya Wazee wetu watoke kwenye usawa na kuwa mabwanyenye, hali ilianza kubadilika kwa haraka sana,wakazaliwa machifu na watemi na kuanza kuweka utawala wao na himaya.
Ghafla kwa kushangaa zaidi wakaanza kuingia wageni kutoka bara la Asia na kukutana na wenyeji, kutokana na mwingiliano huu wa ajabu lugha yetu adhimu ikazaliwa yaani Kiswahili.
Ukaanza utumwa na kutawaliwa na wajerumani kwa mabavu,hakuna lenye mwanzo likakosa kuwa na mwisho, hatimaye Waingereza wakawaondoa Wajerumani na kutawala Nchi baada ya kushinda vita ya dunia.
Wazee hawakutaka kutawaliwa kwa juhudi na maarifa wakaanzisha vuguvugu la kudai uhuru,Mnamo 1961 wakaupata, ikazaliwa nchi ya Tanganyika na visiwa vya Zanzibar vikapata uhuru kwa mapinduzi mwaka 1963. Kwa mipango ya Mungu akazaliwa binti mrembo sana Tanzania kutoka kwenye makucha ya watawala wa kidhalimu.
Binti Tanzania akawa anaongozwa na mwalimu ,mwalimu aliyetufundisha Ujamaa na Kujitegemea, Mwalimu aliyeanzisha Azimio la Arusha, Mwalimu aliyesema na kutufundisha kuwa kuna kung'atuka tofauti na kung'atuliwa kama viongozi wengi wa Afrika walivyoondoka kutoka kwenye viti vyao.
Binti hakuwa mtoto tena akaanza kuwa kijana au kigori, alianza kunawiri kwelikweli kwa kazi kubwa iliyofanywa na Mwalimu kumtunza, akawa na Viwanda vyake, mashamba yake,ranchi zake na vingi alivyobarikiwa na muumba kama madini,maziwa,bahari na Mito inayotiririsha maji nchi nzima.Nchi ikaungana wakazi wote wakawa wamoja.
Baada ya Mwalimu kung'atuka akaingia Mzee wa Ruksa nchi ikafunguka mambo yakawa ruksa kwa kila kitu kuanzia siasa za vyama vingi na vingine vingi,muda ukamtupa mkono mzee ruksa akaingia Mzee wa Lupaso.
Mzee wa lupaso aliingia madarakani binti akiwa na umri wa miaka ya utu uzima karibia miaka 34,binti alikuwa si haba alifika umri wa kuoa au kuolewa.
Mjomba aliamua kumuozesha binti kwa kumuoza jumla jumla kwa kauli ya kubinafsisha, aliozesha mashirika yote ya Umma kwa wenzetu, bila wajomba wengine kujua kiwango cha mahari na wajomba wenzake kujadiliana juu ya kiwango cha posa na mahari ya binti yao, Kijana akaweza kuhimili mfumuko wa bei huku wananchi wengi wakiwa na ukata wa kutosha.
Mzee wa Lupaso akajenga uwanja wa mpira na kuacha alama yake na kutuachia kitabu akilaani juu ya kumuoza binti maana hata yeye hakuwa anajua binti aliozwa kwa kiasi gani.
Zamu ikafika kwa mtanashati au Mzee wa Msoga akawa kiranja mkuu wa kumsimamia binti,kwa ari na kasi mpya binti Tanzania alianza kuzeeka kwa kasi ya ajabu, Dowans, Richmond na ununuzi wa rada ulimfuja binti na kuanza kuzeeka, binti akawa mbibi kwa kipindi hiki,alionekana Mao wa miaka mingi tu.
Mzee wa Msoga alimpa pasi ya upendo mtani wake Tingatinga au mwendazake,mengi yakafunuliwa, Uzalendo ukatamalaki, mtoto demokrasia na haki za binadamu akapata ajali wakafa wote kwa pamoja, tukaanza kumpamba binti kwa mapambo mbalimbali kwa miradi ya kimkakati, tukaanza kumlisha na kumpendezesha binti kwa pesa za ndani na kuambiwa tuwe wazalendo na binti kuozeshwa kwa ndugu zake wa ndani na sio wageni na kuambiwa tuwe wazalendo.
Binti akawa amezeeka kwelikweli na kuwa ajuza, hatazamiki tena,mvuto wote ukawa umekwisha kwa umri wa kuishi kwa binti, barua zote za posa na makubaliano ya ndoa ziliombwa na mwendazake ili kuhakiki uhalali wa ndoa, tukaambiwa tumepigwa na bibi akatakiwa avunje ndoa arudi nyumbani akiwa amezeeka kwelikweli, tuliambiwa bibi hana ndoa halali zote ni uwongo na hazina uhalali wa kisheria.
Tulifurahi sana kama wana ukoo,bibi yetu kurudi nyumbani licha ya kuzeeka,tuliamua kumlea wenyewe bibi yetu na kuanza kufunga mkanda,kwa bahati mbaya mjomba naye akaondoka na kumuachia majukumu yote mama.
TULIPO SASA
Mama kwa majonzi na Msiba mkubwa wa kaka yake akaamua kuwatumia manabii ili wafanye kazi ya kumfufua mtoto demokrasia,utawala wa sheria na haki za binadamu,akaanza kumtafuta mjomba wetu mpendwa aliyepotea aliyejulikana kama maridhiano, lakini pia kwa ujuzi mkubwa aliendelea kumpamba bibi yetu Tanzania ili aonekana kijana kama wenzake, bibi yenye anafanyiwa ukarabati wa hali ya juu kwa ujenzi wa reli ya kisasa, bwawa la umeme la mwalimu wetu na kuingia mkataba kwa ajili ya kuboresha lango la kuingilia nyumbani kwa bibi.
Swali kubwa ni kwanini bibi azeeke kabla ya wakati wake,kwa mfano yule binti aliyepata ndoa mwaka 1777 amekuwa akiendelea kuwa msichana kigori kabisa licha ya ubabe na misukosuko anayepitia kila siku likiwemo lile tukio la kubakwa Septemba 11, ukikaa na bibi anasema miaka ya 1980 alikuwa sawa kabisa na yule ajuza ambaye amekuwa binti na kutikisa uchumi wa dunia licha ya kujitawala mwaka 1949 kwa kupitia uongozi imara wa ule uwanja wa kule visiwani yaani Mao tse tung.
Bibi ni Ajuza licha ya kuwa amezaliwa 1964 , ukienda kwenye vijiwe vya kahawa hadithi kubwa ni kuwa bibi amekuwa ajuza kwa sababu ya kuwa na katiba ambayo imepitwa na wakati,ukiangalia kwa uwanda mpana kuna mengi ya bibi kuwa ajuza kuliko yanayosemwa.
Ushawaza bibi atakuwaje mwaka 2050 au 3000.
Tatizo kubwa la bibi linaanzia kwenye mfumo wake wa utawala, mfumo wake wa utawala amerithi kutoka kwa mkoloni ambapo kwa sasa hauna tija zaidi ya kumuongezea tu mzigo bibi, ushawaza uwepo wa wakuu wa mikoa,wilaya na maDed, maRas, madas, wenyeviti wa halmashauri na mameya pamoja na wabunge unampa bibi mzigo mkubwa sana kiuendeshaji kwanini usipunguzwe ili kuendana na hali ya sasa ya uchumi.
Tatizo lingine la bibi ni uwepo wa tawala za mikoa na serikali za mitaa ambazo hazina ufanisi na kuwa na muundo mgumu wa kiutawala.
Bibi aliamua akili ndogo zitawale akili kubwa,usishangae mtunga sheria na sera anatakiwa ajue kusoma na kuandika tu,wakati msimamiaji anatakiwa awe amekaa darasani kwa kipindi kirefu sana.
Matumizi ya anasa ya bibi nayo ni chanzo cha kumzeesha, hivi unajua bibi sheria yake ya manunuzi anakataza kununua vitu vilivyotumika vinatakiwa vipya tu, na unajua watumishi wa bibi ili wawe na ufanisi wao wanataka kupanda mashangingi tu ambayo ni gharama kubwa sana.
Wajukuu wa bibi pia nao ni changamoto kubwa sana kila mmoja anawaza kuchukua urithi wake hata wale wadogo wakose, wengi wanawaza kuwa matajiri na vyeo vikubwa na sio kuwa na utendaji uliotukuka,Wajukuu wa bibi ambao ni madaktari hawataki kutibu,wauguzi hawataki kuuguza,walimu hawataki kufundisha,wakulima hawataki kulima na wapishi hawataki kupika.
Tuchukulie mfano mdogo kwenye sekta ya afya ambayo kuna uhaba mkubwa wa watumishi, hivi unajua kuna raslimali watu ambazo hazitumiki zipo tu, kila halmashauri ina mganga mkuu ambaye anafanya shughuli za kiutawala kama mganga mkuu wakati hizi kazi angeweza kufanya katibu wa Afya bila shida yoyote, bado kuna kamati za afya za mkoa na halmashauri karibia watumishi wake wote hawafanyi kazi walizosomea zaidi ya kufanya shughuli za uratibu ambazo kuna watu wanaweza kuzifanya. Shida kwa sasa sio wataaalamu au uhaba shida ni namna tunavyowatumia
Kilimo ni uti wa mgongo kwa bibi lakini maafisa ugani wapo mjini wakikusanya mapato na kukaimu utendaji wakati vijijini wakulima wanakosa wataalam.
Kuna haja kuifumua nyumba ya bibi na kuanza moja ili kila mtu awe na majukumu yake,majukumu ambayo watu watalipwa kwa usawa kulingana na muda waliopo kazini na elimu zao bila ya kuangalia yupo wapi.
Ndio Mwalimu wa kule buserere mwenye shahada awe analipwa sawa na mbunge aliyepo bungeni,Waziri mwenye PHD awe analipwa sawa na yule profesa wa kilimo kule SUA Morogoro, ndio na yule mbunge wa darasa la saba awe analipwa sawa na yule mlinzi wa shule kule Nanjilinji,hii itawafanya watu wafanye kazi kwa mapenzi na hamasa kubwa na sio kufuata kipato.
Hii itasaidia sana kuzalisha wataalam na viongozi wenye shauku ya mabadiliko na sio wachumia tumbo.

Upvote
1