Tulisikia toka kwa Rais "Watanzania sio wajinga"

Tulisikia toka kwa Rais "Watanzania sio wajinga"

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2007
Posts
6,630
Reaction score
1,945
Ni kweli Watz. sio wajinga na wana uelewa sana. Ukiangalia mambo yenye akili wayafanyayo kibinafsi utashangaa sana.
Lakini wanasiasa wanawaona hawana akili , wenye akili ni wao tuu.

Wazee wawili kwenye kijiwe chao hapa karibu na kazini kwangu walikuwa wanabishana kuhusu tafsriri ya ughaifu. Mmoja akasema udhaifu ni kinyume cha nguvu. Mfano. Uoga ni udaifu na ni kinyume cha ujasiri. Mwingine akasema .. kwa hiyo ukiwa na nguvu nyingi sana za kiume unaweza ukawa ni udhaifu?
Mwenzake akamjibu, ndio ni ugonjwa na ugonjwa ni udhaifu wa mwili. Ukiwa na nguvu nyingi za kiume ukazitumia kwa mama mmoja si hatamudu? Unahitaji wengi na kila siku ladba. Huo si ugonjwa?

Mwingine akadakia, sasa utajuaje jamaa ana udhaifu wa nguvu hizo. Yaani hana kabisa au anazo sana. Wote wakacheka, lakini mmoja akasema .. sisi wanaume hatauwezi, lakini mwanamke anaweza kukuambia. Yule hawezi au yule amezidi ?

Nilichojifunza toka mazungumzo haya ni kwamba sii rahisi kujitapa kuwa una nguvu hadi mwingine aseme wewe huna nguvu. DHAIFU.
Mwanamke akikumbia hivyo next time utanunua viagra kama nguvu iko down. Lakini viagra haindoi udhaifu. Je kumfukuza Lema na Mdee ndio kudhirihirisha una nguvu?
 
Kudhihirisha ukichaa yaleyale ya bakora za kichwa yanataka kujirudia tusipokua makini atakuja rarua watu kwa meno yake mle ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom