Katiba ya nchi ibadilishwe, muuaji awe anahukumiwa hapo hapo na hakimu kama wanavyohukumiwa wahalifu wengine. Hapa namaanisha kuwa mtu anapohukumiwa kunyongwa basi anyongwe siku hiyo hiyo au apewe wiki/ mwezi mmoja tu, lakin bila kusubiri saini ya raisi.
Hili swala la kusubiri hadi raisi wa nchi asaini hukumu ya kunyongwa muuaji, ndio linasababisha wauaji wengi kuendelea kula bata jela bila hukumu zao kutekelezwa, na hivyo mauaji na vitendo vya kikatili kuendelea kufanyika ktk jamii zetu maana wauji wengi huwa hawahukumiwi.
Tukianza kuhesabu toka hukumu ya kunyongwa ilipotungwa hadi leo wameshahukumiwa wangapi, sidhani kama tutapata hata watu 20. Mfano sidhani kama mwl Nyerere aliwahi kusaini wauaji wangapi wanyongwe, Mwinyi je, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia?
Uzoefu unaonesha kuwa kila raisi anapoingia madarakani hukwepa jukumu hilo la kusaini wauaji kunyongwa, hivyo kufanya wahalifu wasiogope hukumu hiyo maana haitekelezeki. Haiwezekani mtu akipatikana na hatia ya kuiba, kubaka, kupigana, kuuza madawa ya kulevya nk ahukumiwe hapo hapo mahakamani na kuanza kutumikia hukumu yake, halafu muuaji yeye ahukumiwe lkn hukumu yake isubiri saini ya raisi wa nchi ambae hakuwepo wakati hukumu ikitolewa.
Narudia tena, sheria inayohusu adhabu ya kunyongwa kwa wanaopatikana na hatia za mauaji ibadilishwe ili kulinusu taifa na mauaji ya kila siku.