Tumaini university dar es salaam wanatunyanyasa wanafunzi.

Tumaini university dar es salaam wanatunyanyasa wanafunzi.

Tough lady

Senior Member
Joined
Jul 24, 2013
Posts
151
Reaction score
183
Naandika habari hii ili kuwasaidia hata wadogo zetu na ndugu zetu wajue uozo uliopo Tumaini University Dar es salaam,ni chuo ambacho kwanza mazingira yake hayafai kuitwa chuo kikuu, mtu ajaribu kwenda Mwenge barabara ya Coca cola ajionee mazingira tunayosomea, lecture rooms ni jengo la mabati limetengwa kwa ceiling boards, computer room ina computer ila zinazofanya kazi si zaidi ya computer 10, mnaweza kukaa semester ikafika nusu bila lecturer, wakimpata anafundisha miezi 2 halafu mnaambiwa semester tayari kwa somo hilo, hii imewapata sana watu wa education mfano katika course ya Geography na Educational media and technology.Unaweza kuamini haya mambo yanatokea katika chuo ambacho ada yake ni shilingi 2,500,000 kwa mwaka?, miaka 3 ada ya Tumaini dsm ni shilingi 7,500,000.Hayo ni baadhi ya kero za Tumaini university Dsmkwa ufupi.
Tatizo sugu zaidi lililonituma kuandika leo hii ni tatizo la hela ya mkopo toka HESLB.Kama unasoma Tumaini kwa kutegemea hela ya mkopo unakuwa umekwisha, hela ya mkopo Tumaini huwa inatoka wiki 2 hadi 3 baada ya vyuo vingine kupokea hela hizo, tatizo zaidi ni hela za field. Mwaka jana wanafunzi wa education walilipwa shilingi 480,000 badala ya  620,000, kwa maelezo kuwa eti hawakuwa kwenye bajeti ya bodi kwani uongozi haukuonyesha kama kuna field wakati huo, na hizo hela zilipatikana baada ya vikao vingi sana na loan officer wa kipindi hicho...
Sasa, mwaka huu, mpaka sasa hivi, wanafunzi wote wa Tumaini university Dsm, hatujapata hela ya field, na wakati huo field imeanza tangu tarehe 15 july.Wakati tunafunga, tuliambiwa kuwa hela haijaja toka loan board hivo tukapewa karatasi yenye majina tukajaza namba za account ili hela itakapofika toka loan board watuingizie hela kwa kuhakiki account zetu kupitia karatasi tuliyosaini.Cha ajabu, jumatatu iliyopita, tukatumiwa ujumbe kuwa watu tuliopo Dsm tufike chuoni kwa ajili ya kusaini na kuhakiki namba za akaunti kwenye hela ya field, walioweza wakafika wakasaini, cha ajabu, mpaka leo hii, hakuna hela ya field iliyoingia, na je kwa waliopo mkoani, chuo kinafikiria wataishi vipi na wako field?, na kwanini tusipewe hela zetu kwa kuwa tulishaacha akaunti namba wakati wa kuondoka chuo?,hivi sasa kila mtu anasema la kwake, hatuna wa kumuuliza maana hata serikali ya wanafunzi haijulikani kama ipo au haipo, ulifanyika uchaguzi wa serikali, ukapingwa na mgombea aliyeshindwa, kuanzia hapo hatuelewi kinachoendelea.Naandika hivi kwa niaba ya wanafunzi wenzangu, tunaumia sana, naomba wanasiasa na viongozi wa dini waingilie kati, hiki chuo wanadai ni cha dini, lakini wanafunzi tunanyanyaswa tofauti na dini inavotaka watu watende,..kuna mengi sana hapo chuoni, nategemea pia kuanzisha page facebook itakayoeleza uozo wote wa Tumaini, na hiyo page itasaidia wanafunzi wengi kutoa dukuduku lao,nitapost jina la page pindi niianzishapo.
Ni hayo tu kwa leo, naomba jamii itusaidie wanafunzi wa Tumaini, na nawaasa ndugu zangu, ukiamua kujiunga Tumaini Dsm, ujitayarishe kuwa na roho yenye kusononeka kwa miaka yote utakayosoma hapo.

pole sana mkuu, nimewahi kusikia malalamiko kama hayo kwa jamaa yangu anasoma hapo. inasikitisha sana

Kiukweli,Tumaini University Dar es Salaam tawi la Mwenge ni abracadabra! Hakuna mazingira hata ya kuita Shule ya Msingi pale. Kwani mnasomaje kwenye kontena mle?!?

niliposikia Tumaini DSM wamehamia Mwenge nilijua wamejenga kampasi ya kisasa kumbe sivyo!
karibu vyuo vikuu vyote vya Tumaini vina matatizo, mwaka juzi 2011 Tumaini SMMUCO cha Moshi wanafunzi wake waligundua wanafundishwa shahada feki wakalalamika na wakagoma lakini hawakusikilizwa, baadaye wanafunzi wale wakaamua kuacha masomo na kwenda kutafuta vyuo vingine kusoma.

Tunain kwa ujumla wameshindwa sana kwenye Elimu. Ukiona chuo kikuu kina hadhi ya tuition centre.
Haya yanafanyika karibu kabisa na mamlaka ya TCU, najua TCU watasema hawana wataalamu, vifaa, bajei.... Lakini, hata kukagua chuo kilichopo takribani 4km.
Sijui kwenye afya hali ikoje.

Naandika habari hii ili kuwasaidia hata wadogo zetu na ndugu zetu wajue uozo uliopo Tumaini University Dar es salaam,ni chuo ambacho kwanza mazingira yake hayafai kuitwa chuo kikuu, mtu ajaribu kwenda Mwenge barabara ya Coca cola ajionee mazingira tunayosomea, lecture rooms ni jengo la mabati limetengwa kwa ceiling boards, computer room ina computer ila zinazofanya kazi si zaidi ya computer 10, mnaweza kukaa semester ikafika nusu bila lecturer, wakimpata anafundisha miezi 2 halafu mnaambiwa semester tayari kwa somo hilo, hii imewapata sana watu wa education mfano katika course ya Geography na Educational media and technology.Unaweza kuamini haya mambo yanatokea katika chuo ambacho ada yake ni shilingi 2,500,000 kwa mwaka?, miaka 3 ada ya Tumaini dsm ni shilingi 7,500,000.Hayo ni baadhi ya kero za Tumaini university Dsmkwa ufupi.
Tatizo sugu zaidi lililonituma kuandika leo hii ni tatizo la hela ya mkopo toka HESLB.Kama unasoma Tumaini kwa kutegemea hela ya mkopo unakuwa umekwisha, hela ya mkopo Tumaini huwa inatoka wiki 2 hadi 3 baada ya vyuo vingine kupokea hela hizo, tatizo zaidi ni hela za field. Mwaka jana wanafunzi wa education walilipwa shilingi 480,000 badala ya  620,000, kwa maelezo kuwa eti hawakuwa kwenye bajeti ya bodi kwani uongozi haukuonyesha kama kuna field wakati huo, na hizo hela zilipatikana baada ya vikao vingi sana na loan officer wa kipindi hicho...
Sasa, mwaka huu, mpaka sasa hivi, wanafunzi wote wa Tumaini university Dsm, hatujapata hela ya field, na wakati huo field imeanza tangu tarehe 15 july.Wakati tunafunga, tuliambiwa kuwa hela haijaja toka loan board hivo tukapewa karatasi yenye majina tukajaza namba za account ili hela itakapofika toka loan board watuingizie hela kwa kuhakiki account zetu kupitia karatasi tuliyosaini.Cha ajabu, jumatatu iliyopita, tukatumiwa ujumbe kuwa watu tuliopo Dsm tufike chuoni kwa ajili ya kusaini na kuhakiki namba za akaunti kwenye hela ya field, walioweza wakafika wakasaini, cha ajabu, mpaka leo hii, hakuna hela ya field iliyoingia, na je kwa waliopo mkoani, chuo kinafikiria wataishi vipi na wako field?, na kwanini tusipewe hela zetu kwa kuwa tulishaacha akaunti namba wakati wa kuondoka chuo?,hivi sasa kila mtu anasema la kwake, hatuna wa kumuuliza maana hata serikali ya wanafunzi haijulikani kama ipo au haipo, ulifanyika uchaguzi wa serikali, ukapingwa na mgombea aliyeshindwa, kuanzia hapo hatuelewi kinachoendelea.Naandika hivi kwa niaba ya wanafunzi wenzangu, tunaumia sana, naomba wanasiasa na viongozi wa dini waingilie kati, hiki chuo wanadai ni cha dini, lakini wanafunzi tunanyanyaswa tofauti na dini inavotaka watu watende,..kuna mengi sana hapo chuoni, nategemea pia kuanzisha page facebook itakayoeleza uozo wote wa Tumaini, na hiyo page itasaidia wanafunzi wengi kutoa dukuduku lao,nitapost jina la page pindi niianzishapo.
Ni hayo tu kwa leo, naomba jamii itusaidie wanafunzi wa Tumaini, na nawaasa ndugu zangu, ukiamua kujiunga Tumaini Dsm, ujitayarishe kuwa na roho yenye kusononeka kwa miaka yote utakayosoma hapo.
Tough lady pole sana. Kwani Prof Mmari bado mkuu wa chuo? Ombeni kuonana nae yule mzee mwelewa sana atawasaidia. Kuhusu suala la mazingira mnayosomea poleni sana hilo sina la kulisemea kwa sasa. Harakati zako unazotaka kuzifanya nashauri mtumie njia ya mkato kuliko kutumia mitandao ya kijamii (which to some extent inaweza kusaidia) nashauri mjikusanye kama wanafunzi muwaite waandishi wa habari muwaelezee hali halisi ilivyo hapo chuo ila lazima muanze na step 1 ya kuukabili uongozi wa chuo na kuwaelezea matatizo yenu wasiposikia ndo mchukue mkondo huo.
Hakunaga chuo kinachopenda kutoka kwenye magazeti kwa shutuma kama hizo.

Last edited by a moderator:
Mzee Mmmary hayupo tena Tumaini University, mkuu wa chuo mpya hajawahi kutambulishwa rasmi, matangazo kuhusu mambo ya administration mara nyingi yanafanyika katika kipindi cha devotion asubuhi, ambapo nalo ni tatizo lingine la Tumaini, wapo wanafunzi wa dini mbalimbali, lakini matangazo yanatolewa ndani ya kipindi cha dini ambacho si watu wote ni Lutherani.
Swala la kuita watu wa media linakuwa gumu kwa sababu serikali ya wanafunzi kwa wakati mwingine wanakuwa ni kama vibaraka wa uongozi wa chuo unaotunyanyasa,na ndio sababu kubwa ya uchaguzi kuwa na migogoro, maana inaonekana wazi uongozi wa chuo haukutaka serikali iliyokuwepo ipinduliwe.
Watu wengi wa media wanasoma Tumaini na naamini wana uwezo wa kusaidia, lakini hilo lote linategemea na support ya serikali ya wanafunzi..
Ndugu zangu nawashauri hata kama umekosa chuo cha kusoma, usije Tumaini Dsm, wala usimpe mtu ushauri wa kuja chuo hiki maana atakulaumu kwa miaka yote atakayosoma hapa.
madarasa tunatotumia yanatia huruma, ni ceiling board tu, mtu akiwa anatembea juu unamsikia, maana lile godown, wameamua kulitengeneza ghorofa, ambayo inatenganishwa kwa ceiling board kati ya vyumba vya chini na vyumba vya juu,kuna siku watu wa juu watadondokea kwenye vyumba vya chini baada ya ile roof kuzidiwa

Dahh... Inasikitisha sana! Wapi TCU, je University Act, 2005 inasemaje juu ya hili?

Hawa jamaa ni magumashi makumira ndo main campus lkn ada ya makumira ni ndogo kulinganisha ya dar,kambi ya upinzani ilishamulika hichi chuo kuhusu ada ila ndo hivyo tena serikali sikivu inasikia ila haielewi,TCU mko wapi nyie si ndo wasimamizi.

Ninyi ni wazembe, anzisheni kunji! Bodi ya mikopo ni 1km kutoka hapo, TCU ni kama 3km toka hapo. Acheni ujinga

Ninyi ni wazembe, anzisheni kunji! Bodi ya mikopo ni 1km kutoka hapo, TCU ni kama 3km toka hapo. Acheni ujinga

Ni kweli dawa yao kunji tu, ila kama nilivoeleza kwenye post ya kwanza kabisa, sasa hiviv tupo field, tumetawanyika mikoani, hela ndo ipo mikononi mwao sasa hivi,inakuwa ngumu kujikusanya maana hakuna mwanafunzi ambae kapewa hela ya field hadi sasa hivi, sasa wa mikoani watatoka vipi?,,
Mbaya zaidi sasa hivi loan officer anadai kuwa ni mpaka hiyo karatasi ya field money isainiwe na at least nusu ya wanachuo, itasainiwa vipi nusus wakati watu wako mkoani?, ina maana hapo ni ujanja umefanywa na management ili wakae na hizo hela mpaka tutakapofungua chuo, sasa hivi field ndio tuna week 2 tu, na tunafanya field hadi tarehe za mwanzoni za mwezi Sepember, wanadhani watu wataishi vipi?, na kama walijua ni hivo kwanini walitupa karatasi tuandike akaunti namba zetu ili watuingizie hela?,,TUMAINI IS TOO MUCH,ada 2,500,000, lakini oneni mateso tunayopata..

Picha tafadhali

Picha nitaweka anyday, nitakwenda kupiga picha watu waone hayo mazingira ya chuo kikuu kilichopitishwa na TCU yetu,,wakati tunakaribia kwenda likizo wameanza kujenga jengo mle ndani, muda wote tunapishana na malori ya mchanga mle ndani, vyumba vya watu wa education ilikuwa shida kwao, maana kuna mashine ya huyo mkandarasi mchina inapiga kelele masaa yote, na hapohapo, ni nje ya ukuta wa vyumba vya education,,hata mtu akiongea huwezi kumsikia, watu hawawezi kukaa maana kelele zile ni kubwa mno...hiyo ndio Tumaini mdau.

Back
Top Bottom