Tumaini university - makumira huu ni wizi

Tumaini university - makumira huu ni wizi

kakaamiye

Senior Member
Joined
Aug 5, 2009
Posts
179
Reaction score
90
Wana jamvi ninapenda kulalamikia wizi unaofanywa na Tumaini University Arusha (Makumira).

Ilikuwa hiv; mwaka jana kuna dogo alichaguliwa kuanza 1st year, bahati mbaya ni yatima, Mungu si Athumani Higher Education Students' Loans Board (HESLB) wakampatia mkopo in Full, kwa kweli alifurahi sana. Sasa kwenda chuoni Tumaini - Makamira akaambiwa anatakiwa atoe Tsh 500,000 ili afanye registration then HESLB wakipeleka mkopo wao chuo kitamrudishia hela atakayolipa. Hapo nikaanza kujiuliza swali huyu ni yatima kaonekana hawezi kujisomesha leo hiyo laki tano atatoa wapi?. Kilichotokea Dogo akaomba nimsaidie hiyo hela kwakuwa atarudishiwa fedha ikilipwa chuoni. Mwanaume sikuwa na kitu ikabidi nikakope sehemu tena kwa riba ya 20% kwani msaada pekee kwa dogo ilikuwa mimi na bahati mbaya sikuwa na hela wala sikumshtua dogo ila nilikwenda straight kukopa.
Sasa kilichotokea Tumaini wamelipwa na wamesema hawatarejesha ile 500,000 kwakuwa ina kazi nyingine ikiwemo kuwalipa walinzi, toka mwaka jana wanazungusha tu, na sijauliza ni wagapi wanadai huenda wapo wengi.

Swali ninalojiuliza hii ni haki kweli? Ada ya chuo maana yake ni nini? Si inajumuisha vyote hivyo? Inakuwaje wizi huu unafanyika tena kwa walalahoi!

Naomba ushauri hiyo hela itarudishwaje


Tatizo kama hili nimelisikia kwa mtu mwingine ila ni Tumaini Iringa
 
Vyuo vya mchangani hvyo..mwambie huyo dogo ajitahdi katika masomo yake ili siku moja afike chuo kikuu{udsm}
 
Vyuo vya mchangani hvyo..mwambie huyo dogo ajitahdi katika masomo yake ili siku moja afike chuo kikuu{udsm}

Duuh ndo ushauri huo unaoona.... haya Perry Udsm
 
Vyuo vya mchangani hvyo..mwambie huyo dogo ajitahdi katika masomo yake ili siku moja afike chuo kikuu{udsm}

ndo tatizo madogo wa siku iz umeenda udism na kidiv2 unaona ushamaliza kila kitu, wakat mwenzio uyouyo kaenda chuo unachokzarau na div1, na asemi chochote. zarau sio nzur mi nashangaa sana enz zetu myaka 2000 sis wa mzumbe ambao tena ndo ilifaa tujisifu mana bila one inayoeleweka uchaguliw lakin hatukuwai kudharauliwa na wamzumbe! madogo siku iz ulimbuken mwing, mmesahau kwamba elimu inakaa kichwan na sio jina la chuo... kumzarau usiyemjua sio vzur
 
kila chuo kina utaratibu wake mkuu ili ufanye registration, kwa makumira ni 600000 kwa BAED na 500000 kwa cozi nyingine.

mbona cguo cha buhayo ili ufanye registration ni laazima uwe umelipa nusu ya ada ambapo full ada ni karibia milion tatu? hapo hushangai? hiyo 500000 huwa inajumuishwa kwenye ada kwa maana hiyo akitoa hiyo atadaiwa 250000 kwa semester ili kukamilisha ada pekee na sio michango mingine.

kitu kingine umesema kapewa mkopo in full jee ada analipiwa 1500000 na hiyo bodi ya mikopo?

lakini pia mbali na ada kuna michango pale kama bima 100000, teaching practice 100000, ada ya mtihani 50000, computer facilities 30000 na mingine mingi tu.

na ikitokea umezidisha ada huwa inahamishiwa semester inayofuata.

sasa basi kwa majibu ya haraka dogo kakupiga tu hiyo hela na sio swala la kusema ni ya kuwalipa walinzi.
 
Back
Top Bottom