Tumalize mjadala: Sergio Busquets Vs Rodri

Tumalize mjadala: Sergio Busquets Vs Rodri

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Tumalize utata, kiungo cha chini, Sergio Busquets Vs Rodri unaenda na nani kwenye timu yako?
IMG_2299.jpeg
 
Sergio Busquet sitasahau unyambisi wake huyu mwamba. Nimeanza kuangalia El Classico mwaka 2007 baada ya jamaa kuingizwa kwenye timu rasmi alisaidia sana kunogesha hizi game most baada ya kombe la dunia 2010 alipo cement nafasi yake Barca na timu ya taifa. Rodri mnyamwezi ila kwa Sergio atasubiri kidogo
Uongo
Sergio busquets hajaanza kucheza el classico 2007. Timu tu ya wakubwa kaanza msimu wa 2008-09

Btw ndio best defensive midfielder of all time, sababu alikuja na style ya tofauti na ikafanya kazi na kupata mafanikio makubwa sana
 
Nawe unafananisha watu walicheza kwenye vipindi tofauti kwa ajili ya nini? Wasindanishe wachezaji wanaocheza kwenye nyakati moja mkuu.
 
Sergio Busquets ni bora kuliko rodri hadi Sasa, na si rodri tu bali Sergio busquets ndio best defensive midfielder of all time

Busquets ndio amekuja kutransform nafasi ya defensive midfielder, zamani ilionekana lazima iwe ya mtu mwenye miguvu anayetoka sana jasho. Lakini Busquets alikuja na kitu cha tofauti sana, bila kukaba kwa nguvu bila kutoka sana jasho lakini lazima mpoteane

Rodri bado, japo a aweza kuja kumfikia hata kumpita busquets Ila kwa Sasa bado. Busquets amekaa kwenye kiwango Bora kwa miaka 15. Rodri bado bado, angalau aweze kumaintain huu uwezo alionao kwa miaka 10
 
Sijaelewa, yaani rodri ana nguvu kubwa kwenye ulinzi ukimaanisha nn? Tackles? Aerial battles? Au Ni nn?
Takwimu zinaonyesha kuwa Rodri alikuwa na tackles bora zaidi kwa mechi (2.2) ukilinganisha na Busquets (1.3 tackles kwa mechi) katika msimu wa 2021-2022. Hapo nimeongelea tackles mkuu
 
Back
Top Bottom