Tumalize mjadala: Sergio Busquets Vs Rodri

Takwimu zinaonyesha kuwa Rodri alikuwa na tackles bora zaidi kwa mechi (2.2) ukilinganisha na Busquets (1.3 tackles kwa mechi) katika msimu wa 2021-2022. Hapo nimeongelea tackles mkuu
Kwa msimu mmoja tu hukupaswa kumhukumu, pia huo msimu busquets alikua tayari anaenda mwishoni mwa carrier yake. Ni sawa na sasa hivi useme Nico Williams kamzidi Messi kwenye ku-dribble
 
Umemaliza👊
 
Busquets ni Mkubwa kwa Rodri, amecheza mechi nyingi sana kumzidi Rodri....Rodri akifika alipofika Busquets huenda akawa bora zaidi

Kuwalinganisha kwa sasa ni vigumu kwasbb wameoishana idadi za mechi na aina ya Wachezaji waliocheza nao timu moja
 
Kwa msimu mmoja tu hukupaswa kumhukumu, pia huo msimu busquets alikua tayari anaenda mwishoni mwa carrier yake. Ni sawa na sasa hivi useme Nico Williams kamzidi Messi kwenye ku-dribble
Ngoja nichambue kwa sehemu tatu mkuu

Ulinzi: Rodri yupo vizuri zaidi kwenye ulinzi, akionyesha viwango vya juu vya tackles, interceptions, na aerial duels won. Hii ni kwa mujibu wa takwimu nilizofatilia. Busquets, kwa upande mwingine, anaonyesha kiwango cha juu cha clearances, akionyesha uwezo wake wa kusafisha eneo la ulinzi.

Kushambulia: Ingawa Rodri anajaribu zaidi kwa shots (Mashuti ya mbali kwenye kulenga lango), Busquets anaonyesha ubunifu zaidi na ufanisi kwa key passes na assists.

Kupiga Pasi: Busquets anaonyesha usahihi wa juu wa kupiga pasi kwa ujumla, huku Rodri akionyesha uwezo bora wa kupiga mipira mirefu. Busquets pia anaonyesha uwezo wa kupiga pasi za kusonga mbele (progressive passes).

Overall me nikiwekewa Busquets na Rodri nitaenda na Rodri
 
Mmmh, but rodri amecheza game chache sana compared na busquets hivyo takwimu zake zitakua nzuri
 
Sergio busquets akili zaid anatumia ila Rodrigo huwa yuko tough strong katikat akicheza na Fabian Ruiz wanakuwa very solid mm naenda na busquets ana ubunifu wa kuamua mechi
 
Hakuna aliyecheza na Xavi akawa garasa. Usiulize Xavi nani? Utaonekana hujui mpira. Kuna Xavi mmoja tu katk mpira mpka sasa.
 
Miaka ile game za Barca zinaisha Xavi na Iniesta wamepiga pasi 500 ulikuwa unakuta ¾ ya pasi zote zimeanzia kwa Busquets. Jamaa alikuwa habari nyingine aisee.
 
Umeandika vizuri sema kwenye hiyo miaka 15 sergio kua kwenye top perfomance umetupiga labda miaka 10
 
Mimi mwanacatalunya toka spain naondoka na busquet direct yule jamaa alikuwa na ball brain ya kiwango kikubwa mno alimfanya prime yaya toure kuona guardiola anambagua sabb ya rangi...maestro busquet acchaneni nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…