Tumbo la kuhara ukiwa safarini ni habari nyingine aisee

Tumbo la kuhara ukiwa safarini ni habari nyingine aisee

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Jana nilikuwa na safari ya Dsm - Dodoma ndani ya basi la abiria. Ni basi la daraja la tatu, basi la watu wa kawaida tu.

Wakati tunaondoka Magufuli stendi, mvua ilikuwa inanyesha sana. Ndani ya dakika kama 20 tukiwa kwenye mwendo, tumbo likaanza kuunguruma mdogo mdogo. Nikalichukulia poa.

Aisee, gari tulivyokuwa tunatembea muungurumo wa tumbo ukawa mkubwa sana. Tumbo la kuhara.

Nikaomba dreva nishuke nijusaidie, hanielewi, mvua inanyesha na ni maeneo ambayo huwezi kupata choo.

Aisee, nilishuka Mlandizi wao wakaendelea na safari.
 
Kuna siku natoka mbeya-dar tumepanda saul..kuna jamaa alitingwa na tumbo la kuharisha mpaka unamuonea huruma...

Ma mimi nikajifanya naumwa ili kuongeza uzito tulipiga kelele nyingi hadi dereva alipoweka gari kushoto jamaa akateremka..ile anatua chini tu,dereva akanyanyua gari, kiatu
 
tumia dawa inaitwa LOPERAMIDE ukiwa njian utakuja kunishukuru! hii dawa inazuia kuharisha dk 5
 
Back
Top Bottom