Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Leo nimesome sehemu kuwa wabunge wamepinga ripoti ya mto Mara wanataka iundwe "tume huru." Kila mara tumekuwa tunasikia watu wakilalamika kuwa inatakiwa tume huru ya uchaguzi. Ninavyoelewa, tume kikundi cha watu walioteuliwa kufanya shughuli fulani kulingana na hadidu za rejea wanazopewa na chombo kinachowateua. Sasa ninaposikia watu wakisema tume huru, huwa nashindwa kuelewa kwani tume yoyote huunda na chombo fulani na wanapewa hadidu za rejea, kwa hiyo uhuru walionao unabanwa na hadidu za rejea.
Je tunataka tume ambayo inajiandikia hadidu zake za rejea?
Inawezekana sana kuwa watu tunatumia neno "tume huru" kiurahisi tu lakini kwa makosa.
Mafundi wa kiswahili nawapa mada hapaya kuijadili, jeTume Huru ikoje?