Pre GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuanza kuandikisha wananchi wa Morogoro kuanzia Machi 1. Wapigakura 302,752 watarajiwa kuandikishwa!

Pre GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuanza kuandikisha wananchi wa Morogoro kuanzia Machi 1. Wapigakura 302,752 watarajiwa kuandikishwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanza kwa mzunguko wa 12 wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ambao utafanyika mkoani Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga kwa siku saba kuanzia tarehe 01 hadi 07 Machi, 2025.

Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Morogoro leo tarehe 17 Februari, 2025, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji huo utafanyika kwenye mkoa huo na mkoani Tanga kwenye Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga.

“Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 12 kati ya mizunguko 13 ya uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu wa 12 unahusisha mkoa huu wa Morogoro na Mkoa wa Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema mikoa 27 tayari imekamilisha zoezi hilo ambayo ni pamoja na Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma na Singida

Soma pia: Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza kufanya uboreshaji wa daftari mkoani Tanga kuanzia Februari 13, 2025

Ameitaja mikoa mingine kuwa ni Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

“Mikoa miwili ya Pwani na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza inatarajia kukamilisha zoezi hilo tarehe 19 Februari, 2025,” amesema.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndugu Kailima Ramadhani amesema Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 302,752 mkoani Morogoro sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 1,612,952 waliokuwepo kwenye daftari la wapiga kura mwaka 2020.

tumetu.png

Source: Tume Huru Ya Taifa Ya Uchaguzi
 
Back
Top Bottom