Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 1,012
- 2,317
Hivi kila mmoja wetu hapa si anaufahamu angalau kidogo kuhusiana na masuala ya mchezo wa mpira, ni wazi kila mmoja wetu hapa anaufahamu angalau kidogo kuhusiana na masuala ya mchezo wa mpira, hivi katika mchezo wa mpira kama ikitokea mechi halafu ukute refa atakaye chezesha mechi hiyo ukute ndio amechaguliwa tu na miongoni mwa wachezaji kutoka katika timu moja wapo kati ya zinazoshiriki mechi hiyo, je unazani kutakuwa kunausawa hapo. Kwa kweli lazima kunakuwa hakuna usawa wala haki hapo yani inakuwa ni kama vile timu moja imeamua kuweka mpira kwapani, haiwezekani mchezaji wa timu ya upande mmoja pekee amchague refa wa kuchezesha mechi hiyo alafu tutegemee labda mechi hiyo itakuwa na usawa na haki, alafu kwa bahati mbaya sasa refa anayechezesha mechi hiyo huwezi kumhoji wala kumpangia maamuzi yake, yani kiasi kwamba hata akisema hili ni goli basi hakuna wa kumhoji na akisema hili sio goli hakuna wa kubisha, alafu ndio ukute refa huyo amechaguliwa na mmoja wa wachezaji kutoka katika timu moja wapo kati ya zinazoshiriki mechi hiyo. Kwa kweli hapo hakuna haki hata kidogo, ni kama vile timu moja imeamua kuweka mpira kwapani. Sasa katika mfano huo hauna utofauti na kinachoendelea hapa Tanzania kwa sasa kwenye masuala ya uchaguzi.
Katika uhalisia, ndani ya nchi yetu kwa sasa serikali iliyopo madarakani ndiyo Serikali yenye mamlaka ya kutuletea tume huru ya taifa ya uchaguzi ikiongozwa na Rais aliyepo madarakani ambaye pia ni mgombea, ambayo serikali hiyo iliyopo madarakani ni serikali ya chama cha CCM. Hivyo kwasababu hii kwamba serikali iliyopo madarakani ni ya chama cha CCM ina maana tume ya taifa ya uchaguzi itapatikana kutoka katika chama hicho pekee ikiongozwa na mgombea, wakati ukiangalia nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi vya siasa. hapa kwa kweli hatuwezi kusema kwamba tuna tume huru ya taifa ya uchaguzi, kwasababu tume hiyo imepatikana na chama kimoja pekee kunakuwa hakuna haki hapo. Yani ni sawa na refa kuchaguliwa na timu ya upande mmoja pekee kwenye mechi yenye timu nyingi, hapo hatuwezi kusema kuna haki wala usawa wowote kwenye mechi itakayoenda kuchezwa.
Kwa kweli masuala ya uchaguzi wetu nayafananisha na mechi za michezo ya mpira ambapo refa wa kuchezesha mechi hiyo amechaguliwa na timu ya upande mmoja pekee, sasa hapo tunakuwa tuna refa au tuna kocha wa timu hiyo. Kwa kifupi tu tuseme chama kimoja pekee kilichopo madarakani kutuletea tume huru ya taifa ya uchaguzi sio sawa na haiwezekani kabisa kuwa huru, ni sawa na kutuletea wanachama wa chama hicho kisha na kuwabadirisha majina na kuwaita kwamba ni tume huru ya taifa ya uchaguzi, hii nchi yetu sio nchi ya chama kimoja cha siasa, bali sisi tunamfumo wa vyama vingi vya siasa hakutakuwa na haki kama chama kimoja pekee kituletee tume huru ya taifa ya uchaguzi alafu tutegemee kuwa kutakuwa na haki, bali hiyo itakuwa ni tume ya chama hicho kilicho ileta na wala siyo tume huru ya uchaguzi inayojumuisha vyama vyote vya siasa nchini.
Mapendekezo
Hapa nina pendekezo ambalo naamini kuwa litaenda kutupatia tume huru ya taifa ya uchaguzi ya kweli na uwazi kwa wote ambayo itakuwa imeundwa na vyama vyote vya siasa nchini. Pendekezo langu ni kwamba nilikuwa nashauri iundwe kamati ya kudumu itakayoundwa kwa kujumuisha vyama vyote vya siasa nchini, yaani vyama vyote vya siasa vitaunda kamati hiyo, ambapo kamati hiyo ndiyo ituletee tume huru ya taifa ya uchaguzi na sio serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya chama kimoja pekee cha CCM. Kamati hii ndiyo ikatuletee tume huru ya taifa ya uchaguzi, ambapo kuundwa kwa kamati hii kunaweza kupunguza hata mivutano ya kisiasa wakati wa chama fulani kikitangazwa na tume hiyo kushindwa au kushinda nafasi fulani, kila chama hapo kitalidhika kwasababu kutakuwa na uwazi na kwamba vyama vyote vinakuwa vilishiriki kikamilifu kwenye kuunda tume huru ya taifa ya uchaguzi itakayotangaza matokeo kwa sababu vyama vyote vilishiriki kuundwa kwa tume hiyo kupitia kwenye kamati, hivyo kutakuwa na imani ya vyama vya siasa kuhusiana na tume.
Kamati hiyo itakuwa na wawakilishi wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi na itakuwa na uwezo wa kuhoji tume pamoja na kuishtaki mahakamani. Hapa ndio kutapelekea kuwe na usawa kwa wote, uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa tume hiyo. Kamati itasaidia pia kuondoa mivutano yoyote ya kisiasa hasa kwenye matokeo ya uchaguzi kwa sababu kutakuwa na uwazi hata mtu akishindwa uchaguzi basi anajua kabisa kuwa ameshindwa kwa haki. Lakini pia kamati hiyo itakayoundwa itaongeza imani ya wananchi pamoja na wadau mbali mbali wa masuala ya siasa na uchaguzi kuhusiana na tume ya taifa ya uchaguzi, hali inayoweza kuchangia kwa asilimia kubwa pia kukuza demokrasia nchini.
Nashauri jambo hili kwasababu hii nchi ni ya vyama vingi vya siasa basi tume huru ya taifa ya uchaguzi ipatikane pia na vyama vingi vya siasa sio na chama kimoja kama ilivyo kwa sasa kwenye nchi yetu, kwani kwa kufanya hivi kwa asilimia kubwa kunapelekea kusiwe na demokrasia ya kweli na pia kunapoteza maana halisi ya nchi yetu kuwa ya vyama vingi vya siasa.
Hitimisho
Tanzania bora tuitakayo ni ile ambayo tume huru ya taifa ya uchaguzi haitapatikana kutokana na chama kimoja pekee, bali na vyama vyote vya siasa nchini.

Upvote
18