Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele, leo Februari 07, 2025, amekagua mafunzo ya maafisa waandikishaji wasaidizi kutoka Jiji la Tanga na Wilaya ya Muheza, akibaini maandalizi yao kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mafunzo hayo ni maandalizi ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kufanyika katika mikoa ya Tanga na Pwani kuanzia Februari 13 hadi 19,2025.
Jaji Mwambegele amewasisitiza juu ya ushirikishwaji wa wadau wakiwemo wa vyama vya siasa katika kufanikisha zoezi hilo.
View attachment 3227962
Source: TBC Online