EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Hello JF,
Kwanza ni-declare interest: Mimi ni muumini wa kile kinachowezekana hata kama hakifurahishi kuliko kile kinachofurahisha lakini hakiwezekani.
Kutokana na muundo wa tume huru unavyopaswa kuwa, nachelea kuamini kuwa kuna siku chama tawala kitakuja ridhia ipatikane! Muundo wake kwa vyovyote vile utakuwa kiama kwa chama kinachotawala sasa.
Mf. Ikiwa kila chama kitakuwa na mjumbe mmoja kwenye "bodi", upinzani utakuwa na " wajumbe" wengi kuliko chama tawala ambacho kitashindwa kuipelekesha tume kwa maslahi yake. Sidhani kuwa kuna siku watakubali hilo litokee.
Bali "uwazi katika mchakato wa uchaguzi" ndiyo kitu kinaweza piganiwa na kupatikana kwa kuzingatia mazingira ya demokrasia finyu tuliyopo. Hivyo basi napendekeza vyama vikuu vya upinzani kushinikiza mabadiliko ya sheria ya uchaguzi ili kuwe na transparency wakati wote wa zoezi hilo.
Hiki kitu kiliwezekana "kiasi fulani" mwaka 2010. Baada ya serikali kununua "super computer" kwa ajili ya "kukusanya na kuhesabu" kura, iliviita vyama vyote shiriki kuukagua "siku mbili kabla". Mtambo ulibainika kuwa na " kasoro" kwenye ujumuishi wa matokeo, (hii kasoro ilikuja kumgharimu mgombea wa chadema kwa kura zake kugawanyika kwenda kwa wagombea wengine: Lipumba alipata kura ambazo hakupigiwa). Hii ni kwa mujibu wa gazeti la MwanaHalisi.
Kwa wakati ule niliwalaumu chadema (wapinzani halisi kwa wakati ule). Kwani baada ya kila chama kupeleka "IT" wawili kikagua mtambo na kubaini una shida, ni mtu mmoja pekee aliyepigia kelele suala hilo; mgombea wao Slaa, ambaye alipotoa kauli siku mbili kabla ya uchaguzi kuwa ccm wamevuruga uchaguzi, hivyo ufutwe na mchakato uanze upya alionekana hayawani.
Viongozi wa chams walikuwa bize kupigania ubunge kwenye majimbo yao na kumwacha solemba akilia na NEC.
Lengo la huu mfano ni kuonesha kuwa kinachowezakana (kwenye mazingira tuliyopo ya demokrasia hafifu) ni kuisukuma serikali ikubali mchakato wa uchaguzi uwe wa wazi. Ingawa najua kwa wafuasi wa "tume huru" hili halivutii.
Bali tume huru haiwezi kupatikana abadani (rejea kauli ya hivi karibuni ya katibu mkuu wa chama tawala). Sasa ni afadhali kupata kidogo kinachowezekana na kuangalia namna kinavyoweza kutumika kuleta mabadiliko kuliko kusubiria kikubwa ambacho hakitawahi kuja.
Tujadili.