Pre GE2025 Tume Huru ya Uchaguzi yakamilisha mchakato wa kutoa elimu kwa wananchi Zanzibar. Mchakato wa uandikishaji umeanza rasmi leo!

Pre GE2025 Tume Huru ya Uchaguzi yakamilisha mchakato wa kutoa elimu kwa wananchi Zanzibar. Mchakato wa uandikishaji umeanza rasmi leo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kwa wiki karibu yote iliyopita huko visiwani Zanzibar, tume huru ya taifa ya uchaguzi ilikuwa kwenye mchakato mzito wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na namna ya kuhamisha taarifa zao iwapo mwananchi atahitaji.

Baadhi ya sehemu na tawala ambazo tume ilipita kwa ajili kutoa elimu huko visiwani Zanzibar ni pamoja na Majimbo ya Donge na Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja na majimbo ya Mtoni, Welezo, Mfenesini, Mwera na Bububu yaliyopo Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Soma pia: Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutekeleza uboreshaji wa daftari la wapiga kura kisiwani Zanzibar kuanza Oktoba 7 hadi 13, 2024

Tume ilipita kwenye maeneo hayo na mengine mengi ambapo ilitumia magari ya matangazo na vyombo vy habari vya huko visiwani Zanzibar kwa ajili y kuwapa wananchi elimu kuhusu namna ya kujiandikisha.

Siku ya leo Oktoba 7 Tume itaanza rasmi kuwaandikisha wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambapo zoezi hilo linategemea kumalizika Oktoba 13 mwaka huu

Tume Zenji.jpeg


Tume Znz.jpeg


Inec znz.jpeg

Zoezi hilo litahusisha mikoa mitano ya Zanzibar na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Kwa hiyo kama huko Zanzibar, tafadhalini sana nendeni mkajiandikishe ili uweze kutimiza haki yako ya kikatiba.
 
Back
Top Bottom