Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, inatarajia kuandikisha wapigakura wapya 5,586,433 sawa na asilimia 18.7 ya wapigakura 29,754,699 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019 mpaka 2020.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema hayo kwenye mkutano wa tume hiyo na wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Tanga leo Jumamosi Januari Mosi, 2025 na kusema kuwa wapigakura 4,369,531 inatarajiwa wataboresha taarifa zao katika zoezi hilo.
"Amesema kuwa wapigakura 594,494 wanatarajiwa wakuondolewa kwenye daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye daftari hivyo baada ya uboreshaji, inatarajiwa kuwa daftari litakuwa na jumla ya wapiga 34,746,638,"amesema Kailima.