Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora yasema madai ya Mbunge Gekul kumfanyia kijana udhalilishaji hayakuweza kuthibitishwa

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora yasema madai ya Mbunge Gekul kumfanyia kijana udhalilishaji hayakuweza kuthibitishwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema uchunguzi dhidi ya madai ya Mbunge wa Babati (CCM), Pauline Gekul na wenzake kudaiwa kuwafanyia vitendo vya ukatili na udhalilishaji vijana wawili waliokuwa wafanyakazi wake, hayakuweza kuthibitishwa.

Amesema tume hiyo ilifanya uchunguzi wa tuhuma hizo zinazodaiwa kufanywa na Gekul aliyedaiwa kutenda kosa hilo Desemba 2023 kwa Hashim Philemon na Michael Marishamu kwa kuwaingizia chupa sehemu ya haja kubwa ili waseme ukweli, kuhusu kumwekea sumu kwenye chakula na kuweka vitu vya uchawi kwenye hoteli yake ya Paleii Lake View.

Mwenyekiti huyo amesema baada ya uchunguzi, tume kwa kuzingatia maelezo ya watu mbalimbali waliohojiwa na vielelezo ambavyo tume imevipitia haikubaini suala hilo kufanyika.

“Hata hivyo tume ilibaini walalamikaji walizuiliwa kwa muda mrefu wakati wakihojiwa na mlalamikiwa kuhusu tuhuma za kutaka kumwekea sumu (Pauline Gekul) pamoja na kupeleka madawa ya kishirikina katika hoteli yake na hivyo kusababisha walalamikaji kukosa haki yao ya kuwa huru,” amesema Jaji Mwaimu.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom