Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Watanzania wengi wamezungumzia na wanaendelea kuzungumzia mapendekezo au rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Tume niite Tume ya Jaji Warioba kwa nia nzuri tu. Baadhi ya wachangiaji wa mawazo wanaipongeza tume katika maeneo mengi kwa maelezo kuwa imefanya kazi nzuri.
Wengine wanaishambulia Tume kwa maneno makali katika baadhi ya mapendekezo, mojawapo ni mapendekezo ya serikali tatu kwa madai kuwa Watanzania wachache waliohojiwa na tume walizungumzia aina au muundo wa muungano unaofaa.
Kwa sababu hiyo wanadai muungano wa sasa wa serikali mbili hauna tatizo. Lakini tukumbushane kuwa ndani ya muungan o wa serikali mbili, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ilipitisha katiba yake inayokinzana na katiba ya Jamuhuri ya muungano ya Tanzania katika baadhi ya vipengere, hivyo tatizo lipo. Kwa nini Watanzania wachache walichangia mawazo kuhusu aina muungano wanaoupendelea.
Huu ni mtazamo wangu binafsi, kwanza ninajiuliza. 1. Watanzania wangapi wanaujua muungano na wenye maslahi ya moja kwa moja kwenye muungano? 2. Watanzania wangapi wa sasa wanauelewa kwa mapana na marefu muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mnyiramba mkulima anayeishi Mtekente au Munkonze jimboni kwa Mh. Nchemba, ninaamini hajui na hana maslahi ya moja kwa moja na muungano. Kuwepo au kutokuwepo muungano kwake yote sawa. Kwake yeye Katiba mpya ingemwezesha kupatiwa maji safi na salama, miungombinu ya barabara, huduma nzuri na bora za afya na mashule yenye Walimu wa kutosha na vitendea kazi ingebadilisha maisha yake.
Tembelea vijijini ujionee mambo.
Makundi yenye maslahi ya moja kwa moja kwenye muungano ni pamoja na Wanasiasa, Wanaharakati, Wafanyabiashara wakubwa na wenye ndugu wanaoishi upande wa pili wa muungano.
Hivyo mimi ninaona ni sahihi kuwa na wachangiaji wachache kuhusu aina ya muungano. Hii haina tofauti kubwa na wachangiaji wachache kwenye Uraia wa nchi mbili kwa sababu, hebu fikiria mkulima na mfugaji wa kijiji cha Lukomo au Kinyangiri huko Singida, mwenye elimu ya darasa la saba, lini ataota ndoto ya yeye kuwa raia wa nchi mbili wakati hana hata cheti chake cha kuzaliwa na haoni umuhimu wa kuwa nacho. Sioni sababu ya msingi ya kuilaumu Tume kiasi hicho.
TUKUBALI YAISHE NA MAISHA YAENDELEE.