Tume ya katiba haikuwaelewa wananchi kuhusu deni la Taifa!

Tume ya katiba haikuwaelewa wananchi kuhusu deni la Taifa!

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Ni dhahiri Tume ya mabadiliko ya katiba inayoongwa na Jaji Joseph S.Warioba imefanya kazi kubwa ya kukusanya,kuyachambua na kuyatoa maoni ya wananchi kupitia rasimu ya katiba mpya. Kwa maoni yangu, kuhusu kipengele cha mikopo na deni la taifa tume haikuwaelewa wananchi na ndiyo maana kuna udhaifu katika mapendekezo ya tume. Binafsi nilitaka kuwepo na chombo maalumu cha kusimamia uhalali,matumizi na ukomo wa nchi kukopa na wala siyo wananchi kupewa taarifa na serikali kupitia bunge. Katika hotuba yake Jaji Warioba alisema..."Wananchi walizungumzia suala la uwepo wa ukomo wa nchi kukopa na uwepo wa utaratibu wa kulipa deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa.Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, Tume imependekeza kuwa, serikali itawajibika kutoa Taarifa Bungeni..." Naona mapungufu hapa, je, hili litatusaidia?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom