Nasubiri kuona kama wataacha hayo magari,lakini hata nyumba,wao wanapaswa kuzunguka nchi nzima na si kuka kwenye hizo nyumba.
Nikija kwenye magari,serikali inamagari mengi sana,kunasababu ya kununua mapya,kwanini wasitumie magari ya wizara.
ni jambo la kusikitisha sana,pale wajumbe wanapokuja kutumikia nafasi yao kwa kulinda heshima na marupurupu waliyonayo,badala ya kutumikia hoja zawananchi.
Kwangu mimi kupewa nyumba na gari ni rushwa,wengi watapaswa kutumikia nyazifa hiyo badala ya kazi maalum waliyopewa,na hapa ndipo uwajibibikaji utakuwa tatizo.
Nimeleta hapa tujadili na kutuma ujumbe kwa wahusika.
jambo la msingi hawa wajumbe kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria iliyowaweka hapo, lakini hebu fikiria wale kutoka mikoani mnataka walale nje? Au watembee kwa miguu au daladala zetu za kugombea? Hata heshima na hadhi waliyopewa na rais haitaonekana na kuthaminika.
Yuwaombe wateule hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuwasaidia watanzania wenzao ambao wameweka matumaini makubwa kwao. Tunataka katiba mpya yenye maslahi kwa taifa letu na sio kujadili eti kupewa nyenzo za kazi kuwa rushwa!!!!!